https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    MAMBO 11 YA KUVUTIA USIYOYAJUA KUTOKA KWA WABABE WA CHELSEA

    Crystal PalaceSalym Juma
    Kama jana ule ufunguzi wa kampeni za wale jamaa wanaojiita ‘Makanda’ ungekuwa ni mchezo wa soka, bila shaka ‘Man of the match’ angekuwa yule waziri mkuu wa zamani aliyefanya kazi na yule raisi aliyewaita
    wapinzani ‘Malofa’ na kupigiwa kelele na watu kibao wanao ithamini ile maana sahihi ya demokrasia. Ebwana yule waziri mkuu ni hatari ndio maana mimi sipendi kabisa siasa. Anyway mbali na hayo ya siasa, vipi
    tena ndugu zangu wa Chelsea na Liverpool? Msilaumu huo ndio mpira sio kila siku nyie.
    Bila shaka baada ya makundi ya ligi ya mabingwa kupangwa wiki hii, watu wengi walihamishia macho na masikio yao kule Monaco. Wikiendi hii mambo ya UEFA yalififia baada ya baadhi ya timu kuvurunda tofauti na
    ilivyotarajiwa. Crystal Palace iliisimamisha Chelsea kwa mara nyingine baada ya kuchukua pointi mbele ya Jose Mourinho tena pale darajani. Leo hii naomba ufahamu mambo ambayo pengine hukuwahi kuyafahamu dhidi ya timu hii, karibu sana….
     Crystal Palace ndiyo timu inayoshikilia rekodi ya kushuka daraja msimu uliofuata baada ya kumaliza ‘Top 4’ Hii ilitokea msimu wa 1994/95 wakati namba ya timu zinazoshiriki ligi kuu ya Uingereza ilipopunguzwa kutoka 22 hadi 20 na mkasa huu ukawakumba wababe hawa wa timu kubwa.
    Tangu mwaka 2003, Crystal Palace imekuwa timu pekee ya michezo kuutumia uwanja wa Selhurst Park wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 26, 255  baada ya AFC Wimbledon, timu inayoshiriki madaraja ya chini
    kuhamia Milton Keynes. Kabla ya hapo walikuwa wanautumia uwanja huu pamoja.
    Crystal Palace bado inashikilia rekodi ya timu iliyoteremka daraja mara nyingi ambayo inashiriki ligi kuu ya Uingereza hadi sasa. Wameteremka daraja mara nne kwani walifanya hivyo mwaka 1993, 1995, 1998
    na mwaka 2005. Kumbuka hii ni tangu mwaka 1992 Premier ilipobadilika.
     Uwanja wa Crystal Palace pia bado unashikilia rekodi ya kuwa kiwanja kutoka Uingereza kilichoandaa mechi ambazo zilitazamwa na Wachina Millioni 100 mwaka 1998. Hii ilikuwa baada ya kuwasajili wachezaji wa Kichina kwa mara ya kwanza kucheza Primia, Sun Jihai na Fan Zhiyi walisajiliwa na Palace mwaka 1998 na Televisheni za Kichina kuvutiwa na usajili huu.
    Crystal Palace ndiyo timu ya kwanza kutoka London kucheza na Real Madrid katika jiji la London. Hii ilikuwa mwaka 1962 ambapo walicheza mechi ya kirafiki na timu hii kubwa kabisa barani Uaya na duniani kwa
    ujumla.
    Mara nyingi sana timu hii inapocheza na timu za London, neno ‘derby’ halitajwi sana hii ni kutokana na Crystal Palace kupatikana kusini kabisa mwa London, sehemu ambayo zinapatikana timu za Millwall na Charlton Athletc. Kwa maana hiyo ‘derby’ kubwa inayopatikana huku ni wakati timu hizi zinapokutana.
    Kwa sasa timu hii inamilikiwa na wafanya biashara wanne wa Kimarekani ambao kwa pamoja wanamiliki kampuni ya CPFC 2010 yenye mamlaka ya kusimamia kila kitu ndani ya timu hii zikiwemo shughuli mbalimbali kama kuuza vifaa vyenye nembo ya timu. John Bostock ndiye mchezaji wa Crystal Palace anayeshikilia rekodi
    ya kucheza Primia akiwa na umri mdogo mwaka 2007 pale alipokuwa na 15. Kama wewe ni mfuatiliaji wa EPL utakumbuka kwenye mechi ya Crystal Palace dhidi ya Watford mwezi October. Victor Moses pia amewahi
    kucheza mapema kwenye timu hii akiwa na miaka 16.
    Jezi za timu hii zinadhaminiwa na kampuni ya Kamari inayoitwa Mansion.com. Kampuni hii inapatikana kwenye nchi ya Gibraltar anapotoka aliyekuwa Daktari wa Chelsea Eva Carneiro. Pia kampuni hii
    inadhamini timu nyingine ya EPL ya AFC Bournemouth na hapo awali iliwahi kuizamini timu nyingine ya London ya Tottenham Hotspurs.
     Usajili mkubwa kufanywa na timu hii ni ule wa Yohan Cabaye kwa kitita cha £10m kutoka Paris Saint-Germain msimu huu. Pia kitita kikubwa walichopokea ni kile cha £15 Millioni kutoka kwa Manchester United pale walipomuuza Wilfred Zaha kwenda Old Trafford mwaka 2013.
    Crystal Palace pia inajivunia Academy yake kwa kuwatoa wachezaji mahiri wenye majina makubwa hadi sasa. Kumbuka Wilfred Zaha, Nathaniel Clyne na Victor Moses ni baadhi ya wachezaji walioanza maisha yao kwenye timu hii inayonolewa na Alan Pardew, mchezaji wa zamani wa timu hii.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAMBO 11 YA KUVUTIA USIYOYAJUA KUTOKA KWA WABABE WA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top