Mara nyingi ukienda kutazama
mechi ya watani wa jadi wa Tanzania, Simba na Yanga ni kawaida kuona
mashabiki wa timu hizo wakichana jezi za wapinzani wao mara
wanapothubutu kukaa au kupita eneo lao.
Shabiki mwenye rangi nyekundu
na nyeupe anayekaa jukwaa la kaskazini la uwanja wa Taifa, hawezi
kukatiza eneo la kusini wanapokaa Yanga wenye rangi za kijani na njano.
Kama unadhani huu ni uhasimu mkubwa, basi unajidanganya.
Huko Poland ilikuwa inapigwa mechi kati ya timu ya Zaglebie Sosnowiec na GKS Katowice.
Mashabiki wa Zaglebie Sosnowiec waliamua kumvua nguo shabiki wa GKS Katowice ikiwa ni adhabu baada ya kumkuta amekaa eneo lao.
Tofauti na utamaduni wa kumpiga shabiki anayefanya hivyo, walimuamuru avue nguo zote na kumwacha aende zake.
Shabiki huyo alijihidi kuziba
nyeti zake na kubeba vitu vyake ikiwemo Simu na Wallet, lakini jamaa
wakachukua vyote na kumuacha bila mtupu, kisha wakamwambia potea haraka.
Tazama video hapa chini:


0 comments:
Post a Comment