Mara baada ya mechi kati ya Manchester United Vs Liverpool kama ilivyo ada ya mashabiki mbalimbali wa soka hujisogeza kwenye hotel maarufu pembeni ya Uwanja wa Old Trafford. Basi na mimi nikajisogeza humo ndani kujumuika na watu mbalimbali.
Hotel football ni hotel yenye nyota 4 ikiwa na vyumba 133 na view ya uwanja wa Old Trafford ambayo inamilikiwa na Gary Neville na Ryan Giggs na support ya wachezaji wenzao Paul Scholes, Nicky Butt na Philip Neville.
Nikiwa chini sehemu ambayo wanaingia mashabiki wengi panaitwa Old Trafford Supporters Club. Hapo chini kuna mabishano ya hapa na pale kuhusu mechi pamoja watu wakicheza pool table, TV Screen zikonyesha mechi ya Barcelona na misosi mbalimbali bila kusahau beer za kutosha kwa wanaotumia.
Pia kuna sehemu nyingine high class inaitwa Cafe Football ambayo ina restaurant. Hapo wanaongia watu mbalimbali wa hali ya juu, hapa wale watu ambao niliwaona wamekaa ndani ya Old Trafford kwenye VIP seats wanaingia kwenye hii restaurant.
Mimi nikiwa zangu pake chini kwenye Old Trafford supporters Club, nimekamata zangu burger inaitwa The Boss Burger ambayo imepewa jina kwa heshima ya Boss wa zamani wa Manchester Sir Alex Ferguson ambayo ina nyama kavu na mambo mengine mazuri hata siwezi kuelezea utamu wake.
Sehemu moja ambayo niliambiwa na mhudumu wa hitel hii inaitwa Heaven. Hii ni sehemu ya juu ya hotel. Huko kuna uwanja mdogo.Mhudumu huyo pia aliniambia baadhi ya vyumba vina ukuta wa kioo ambacho usiku utaweza kupata view nzuri ya uwanja wa Old Trafford.
Kwa haraka hii ni biashara kubwa sana kwa wamiliki wake hasa siku za mechi kubwa ilivyokua leo. Idadi ya watu ninano waona hapa na jinsi wanavyotumia pesa, huenda hizi bar zao zinaingiza pesa nyingi kuliko hata hivyo vyumba vyao.
Mhudumu huyu anaendelea kuniambia kwamba kwa mashabiki wa Manchester hujiskia fahari kuja kwenye Hotel Football kwasababu pia ipo karibu na Old Trafford, lakini kitu kikubwa ni kwamba inamilikwa na wachezaji wa Manchester united.


0 comments:
Post a Comment