https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    MBATIA AONGEA KUJIBU ALIYOSEMA DR. SLAA






    Mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia ameongea mchana huu na waandishi wa habari na kujibu baadhi ya tuhuma za Dr. Slaa
    Mbatia: Napenda kuwaomba Watanzania tusimame wote kupata Katiba mpya ambayo ndiyo ajenda ya mgombea wetu Lowassa.
    Mbatia: Watanzania naomba waelewe UKAWA tunasimamia utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji ndani ya Tanzania.
    Mbatia: Wanasiasa hasa wale wa CCM Mwakyembe na Sita, wanaotaka midahalo waje waongee na mimi wasimsumbue Mgombea wetu Lowassa sio saizi yao.
    Mbatia: Hivi ni ashiria kwamba CCM wameshindwa hoja, mara kuleta mambo ya udini, mara wanaibua hili mara lile. wanataka kuchafua amani yetu kwa kuigiza masuala ya dini
    Mbatia: Wagombea wetu urais walikaa na Dokta Slaa alisema mimi ni bora kuliko wote,leo hii anasema hajawahi kutia nia,kweli?
    Mbatia: Tukisema tuibue masuala yote na kashifa za kuuzwa kwa nyumba, kuna mtu atabaki salama?
    Mbatia: Eti Lowassa akija ndani ya Ukawa atakuja na Wenyeviti wa CCM..hakuwahi kusema..kayasemea wapi?
    Mbatia: Wewe unasema ni muadilifu ulipewa Milioni 500 mwaka 2008 unakuja kusema leo baada ya miaka 7? Tuwe wakweli.
    Mbatia: Eti suala la rushwa zaidi ya miaka 7 usiripoti halafu uje useme leo, kusema uongo ni kazi sana.
    Mbatia: Napenda kuwaomba watanzania wote ambao ni zaidi ya milioni 46, wasiruhusu nchi yetu ikaharibiwa na watu 100.
    Mbatia: Wakenya walisema hata kama ana makosa, walisema huyo huyo tunamtaka, wakampigia kura na leo ni Rais wao.
    Mbatia: Watu wachache wanaotaka eti kwa lolote lile lazima waendelee kubaki madarakani, tunasema hapana.
    Mbatia: Lazima tufute mfumo huu uondoke tuwe na Tanzania mpya.
    Mbatia: Napenda kuwaomba wale Viongozi wa dini walionewa kwa yale ya jana, wasamehe na waachane nayo.
    Mbatia: Lowassa hajawahi kutamka kuwa nikija ndani ya UKAWA nitakuja na wabunge 50, wenyeviti wa CCM na Makatibu nk.
    Mbatia: Kama hana faida haya mafuriko tungepata wapi? Nyota ya Lowassa inang'aa hata wafanye nini hawamuwezi huyu jamaa
    Mbatia: Hatuna haja ya kuanza kumjadili, hiyo ni kulipasua Taifa la Tanzania kwa maslahi binafsi
    Mbatia: Kilichotusikitisha ni yeye kuhusisha watu wengine wasiohusika kwenye jamii yetu, viongozi wa dini wenye heshima zao, acha sisi vyama vya siasa tusuguane wenyewe.
    Mbatia: Zimebaki siku 50 na kitu, haki itendeki na nchi yetu ibaki na amani siku zote
    Mbatia: Anasema kaja kupambana na Lowassa kwakuwa anagombea urais, sasa Sumaye naye anagombea urais?
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MBATIA AONGEA KUJIBU ALIYOSEMA DR. SLAA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top