Baada ya Yanga jana kuibuka na
ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Taifa, afisa habari
wa klabu ya hiyo Jerry Muro leo amemtupia kijembe mwenyekiti wa kamati
ya usajili ya Simba Hans Poppe kwa kusema tangu sasa atakuwa akiitwa
Hans Pole na si Hans Poppe kama ilivyozoeleka.
Muro ameto kijembe hicho leo wakati akizungumza na vyombo vya habari kwenye makao makuu ya Yanga mtaa wa Jangwani.
“Tulisikia wenzetu wametuandalia
supu ya mawe na kachumbari ya miiba, mimi nadhani sasa ufike wakati wa
kufungua macho na kuangalia, jana Mkwasa alisema ile supu
waliyotuandalia walionja wao kwanza ikawamaliza”, amekejeli Muro.
“Kwahiyo kwa mzee wangu mimi
nimpe pole na sisi kwetu tangu jana tunamwita Hans Pole sio Hans Poppe.
Najua anaumia ila mimi siwezi kumjibu kwasababu ni mtu mzima sawa na
baba yangu amenizidi umri”.
“Namuombea Mungu aishi miaka
mingi ili aone tunachokifanya, nadhani sasahivi sukari na presha viko
juu ila sisi tunampa pole akae sawasawa ajipange na ajichunguze”.


0 comments:
Post a Comment