https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    SIMBA MAMBO SAFI….YAENDELEZA ‘DOZI’ MKWAKWANI

    Wachezaji wa wa Simba wakishangilia kwa pamoja goli lililofungwa na Hamisi Kiiza
    Wachezaji wa wa Simba wakishangilia kwa pamoja goli lililofungwa na Hamisi Kiiza
    Kivumbi cha Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, leo kimeendea tena na kushuhudia michezo kadhaa ikipigwa, ambapo jijini Tanga katika uwanja wa Mkwakwani, wenyeji Mgambo JKT walikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba SC.
    Mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta nikuvute, ilishuhudiwa timu zote zikishambuliana kwa zamu, huku sehemu ya katikati mwa uwanja kukiwa na shughuli pevu kutokana na viungo wote kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu.
    Simba walikosa bao la wazi kupitia kwa kiungo mshambuliaji wao wa kimataifa wa Zimabwe Justice Majabvi, baada ya kuunganisha mpira mzuri kutoka kwa beki wa kulia wa timu hiyo Hassan Kessy na mpira huo kutoka nje ya lango la Mgambo.
    Krosi iliyopigwa na beki wa kushoto wa Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ilitua moja kwa moja kichwani mwa Justice Majabvi na kuiandikia Simba bao la kwanza.
    Hamis Kiiza aliiandikia Simba bao la pili mnamo dakika ya 73 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Mgambo na kufanikiwa kupata upenyo wa kuutumbukiza mpira huo kimiani na kuamsha nderemo kwa mashabiki wa Simba waliojitokeza uwanja wa Mkwakwani.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIMBA MAMBO SAFI….YAENDELEZA ‘DOZI’ MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top