Timu ya taifa ya Chile imepata
ushindi wake wa kwanza dhidi ya Brazil baada ya miaka 15 kupita mabao
yaliyofungwa na Eduardo Vargas pamoja na Alexis Sanchez.
Katika mchezo huo Chile imefanikiwa
kuifunga Brazil mabao 2-0 katika mchezo wa awali wa kuwania kufuzu
kutinga fainalia za kombe la dunia.
Baada ya kipindi cha kwaza kuisha
bila kuona nyavu zikitingishwa Eduardo Vargas aliipatia Chile bao
kwanza kwa mkwaju wa adhabu katika dakika ya 72 na kisha baadae
Sanchez kupachika bao la pili.
0 comments:
Post a Comment