Ofisi ya rais wa Kenya imetumia
shilingi bilioni 1.4 za Kenya kati ya shilingi bilioni 6.3 za bajeti
yake katika mwaka wa fedha ulioisha kwa shughuli za ukarimu, mikutano
pamoja pamoja na huduma za vyakula kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi wa
Bajeti.
Idara hiyo ya ofisi ya rais ilikuwa
wakati huo ikisimamia ofisi ya rais na naibu rais, ambapo kwa pamoja
zimetumia shilingi bilioni 4.3 za Kenya kwa shughuli za ukarimu,
mikutano pamoja pamoja na huduma za vyakula.
Ripoti hiyo pia imebainisha kuwa
ofisi ya rais imetumia shilingi milioni 203 kwa safari za nje ya
nchi.
Rais Uhuru Kenyatta ambaye
hajamaliza muhula wa kwanza inasemekana ameweka historia kwa kufanya
safari mara mbili zaidi ya alizofanya rais aliyepita Mwai Kibaki
katika mihula yake miwili ya urais.
0 comments:
Post a Comment