Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Ludewa Bw Stanley Kolimba akiweka shada la maua
katika kaburi ya mwenyekiti wa DP mchungaji Mtikila jana.
Viongozi wa Kitaifa wa DP na Mkoa wa Iringa na Njombe wakiwa katika kaburi la Mtikila.
Mwanahabari Francis Godwin wa pili kushoto akimhoji naibu katibu mkuu wa DP Taifa Bw Abduli Mluya juu ya kifo cha Mtikila.
Wananchi wa kijiji cha Milo Ludewa wakitazama Chopa aliyotumia Deo Filikunjombe kufika msibani hapo jana.
ACT Wazalendo na DP waungana katika msiba wa Mtikila.Mwenyekiti
wa DP Mkoa wa Iringa na mgombea ubunge jimbola Iringa mjini Robart
Kisinini kushoto akiungana kubeba jeneza lenye mwili wa Mtikila.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk
Rehema Nchimbi kulia akiwa na Deo Filikunjombe mgombea ubunge jimbo la
Ludewa na mbunge aliyemaliza muda wake katikati kushoto ni msajili wa
vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi jana wakati wa mazishi ya
Mchungaji MtikilaMchungaji Patrick Mgaya aliyekuwa safari moja na marehemu Mtikila wa pili kulia akiwa katika mazishi hayoWaombolezaji wakiwa msibani
Filikunjombe akitoa salamu zake wakati wa mazishi ya MtikilaWananchi wakimsikiliza Filikunjombe
Filikunjombe akitoa salamu zake wakati wa mazishi ya MtikilaWananchi wakimsikiliza Filikunjombe
Filikunjombea akitoa mkono wa pole kwa wafiwa katikaati ni mjane Bi Jojina Mtikila
Filikunjombe akiwasili msibani kwa chopa.
Filikunjombe akiwasili msibani kwa chopa.
Jaji Francis Mutungi kushoto Bw Mgaya na Askofu Mtetemela na Filikunjombe wakiwa msibani
VILIO vilitawala wakati wa mazishi ya
aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha DP, mchungaji Christopher Mtikila
aliyezikwa jana Alhamis kijijini kwao Milo, Wilaya ya Ludewa mkoani
Njombe, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe na Msajili
wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi walitoa ya Moyoni
wakisema alikuwa kiungo mhimu katika Taifa .
Wakati Msajili wa vyama vya siasa nchini
Jaji Mutungi akiwataka watanzania hasa viongozi wa vyama vya siasa
kumuenzi Mchungaji Mtikila kwa kuenzi Amani wakati huu wa kuelekea
katika uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu, Filikunjombe asema mbali ya
ukorofi wa Mtikila kwa kile alichokiamini ila kwake alikuwa ni mshauri
mkubwa wa Ubunge wake katika jimbo la Ludewa.
Wakitoa salamu za rambi rambi wakati wa
mazishi hayo yaliyofanyika leo kijijini kwake Milo Wilaya ya Ludewa,
Jaji Mutungi alisema kuwa katika Enzi zake marehemu Mtikila alikuwa
akisimamia kile anachokiamini. Alisema kuwa mbali ya misimamo yake ya
kusimamia alichokiamini bado alikuwa ni mtu wa kujenga hoja na
ambae hakupenda kuhatarisha Amani ya nchi hakuwa anapenda njia za
mkato katika kupata majibu ya kile asichokiamini.
” Njia za mkato marehemu hakupenda
kabisa kwani hata Kama jambo la kutisha ambalo wengine huogopa yeye
alikuwa tayari kwenda mahakamani kusaka Haki yake bila kuhatarisha Amani
ya nchi Mimi nafikiri kila mmoja akafuata misingi yake katika kudai
Haki bila kuvuruga amani naamini tutafanikiwa “
Alisema kuwa kuna mapungufu yanaweza
kujitokeza ila Jambo la msingi kila mmoja kutanguliza kwanza amani ya
nchi badala kuipa kisogo Amani na kupenda machafuko katika nchi” Hivyo
aliwataka watanzania bila kujali itikadi zao za vyama kuendelea na siasa
huku wakitanguliza Amani ya nchi.
Mbunge aliyemaliza muda wake wa jimbo la
Ludewa ambae ni mgombea Ubunge wa jimbo hilo Bw Filikunjombe alisema
kuwa pamoja na Mchungaji Mtikila enzi za uhai wake alisimamia jambo
ambalo alikuwa akiamini ila kwake amekuwa msaada mkubwa katika ushauri
wa kuwatumikia wananchi wa Ludewa .
Alisema Mchungaji Mtikila hakuwa tayari
kumuunga mkono mbunge wa Ludewa ambae hakuwa msaada wa kimaendeleo kwa
wananchi ila kwa upande wake alikuwa akimuunga mkono na hata
kutosimamisha mgombea katika jimbo la Ludewa. “
Mchungaji Mtikila hakuwa tayari kuungana
na mbunge asiyefanya Kazi za maendeleo jimboni Ludewa ila kwangu
alikuwa akiniunga mkono na hata kunipingeza kwa Kazi nzuri ….. Kicho
chake ni pigo kubwa kwa Taifa hasa kwa wana Ludewa ambao tulijivunia
sana uwepo wake” Hata hivyo alisema njia pekee kwake ya kumuenzi
Mchungaji Mtikila ni kuendelea kuwatumikia vema wananchi wa Ludewa kwa
kuleta maendeleo zaidi Kama alivyohitaji katika uhai wake.
Filikunjombe alisema katika kuamini
kwake na kusimamia anachokiamini hadi mauti inamkuta alikuwa akitetea
kuwepo kwa nchi ya Tanganyika na ndio maana kazikwa na bendera ya
Tanganyika na kudai kuwa hakuna na kosa kupigania Tanganyika kwani
Tanganyika inahitajika.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr Rerema Nchimbi
alisema kuwa Mkoa wa Njombe umepoteza kiongozi makini na kuwa katika
kumuenzi ni vema kwa vyama vya siasa kuendesha kampeni za amani na
utulivu zaidi na kuwa wakati taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu ni
vema kila chama kumuenzi Mtikila kwa kulinda Amani .
Naibu Katibu mkuu wa DP Taifa
Abdul Mluya alisema kuwa suala la kifo cha mwenyekiti wake ni utata
mtupu na bado wanaendelea kuchunguza.
Wakati huo huo Chopa ya Filikunjombe
aliyotumia kufaria kwenda katika mazishi hayo iliwafanya wananchi kuacha
kusikiliza Salam mbali mbali za viongozi na kukimbilia kutazama na
kumlaki Mgombea huyo Ubunge jimbo la Ludewa.
Na MatukiodaimaBlog
0 comments:
Post a Comment