Na Hemed Kivuyo
MWENYEKITI wa kamati ya usajili
ya timu ya soka ya Simba Zacharia Hans Poppe amesema kuwa uongozi wa
timu hiyo haupaswi kulaumiwa baada ya kufungwa kwa 1-0 na Tanzania
Prisons ya Mbeya na hata kuachwa kwa Mchezaji Elius Maguli uongozi
hauhusiki.
Akiongea na Mwandishi wa Habari
hii Poppe amesema kuwa mara kadhaa timu inapofanya vibaya ama kupoteza
mchezo hata mmoja ndipo maswali yanakuwa mengi na wengie hutupia shutuma
viongozi jambo ambalo alidai si sahihi.
Kuhusu usajili Kiongozi huyo
amedai kuwa yeye ndiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na huwa hasajili
bila kupokea mapendekezo ama kupewa majina ya wachezaji
wanaotakiwa kutoka kwa benchi la ufundi la kamati inayohusika.
Ameongeza kuwa suala la timu
kufanya vibaya ama kupoteza mchezo mmoja ama miwili litazamwe kwa
mapana hasa wahusika ambao ni waalimu lakini viongozi walishafanya kazi
yao ambayo nikusajili wachezaji waliyotakiwa na sasa imebaki kazi ya
waalimu ndani ya uwanja.
“Sisi kama viongozi na mimi
nikiwemo huwa hatusajili tu kwa kukurupuka, huwa tunasubiri majina ama
mapendekezo ya wahusika ambao ndiyo wataalam wa soka na tunafanya
hivyo, hutokea mara chache tunashindwa kutimiza matakwa yao lakini kwa
98% tunatimiza kuwapa wachezaji wanaowataka”, Alisema Hanspope.
Kuhusu kuachwa kwa mshambulizi
Elius Maguli ambaye kwasasa anaichezea Stand ya Shinganya na kuwa na
mabao nane,Poppe amedai kuwa kuachwa kwa mchezaji huyo kulitokana na
mapendekezo ya kocha na ni vyema akaulizwa mwalimu.
“Hili jambo la kusema uongozi
ulifanya makosa kuamuacha Maguli sijui linatoka wapi, hivi sisi viongozi
tuna taaluma gani ya ukocha mpaka tumuache fulani au tumsajili fulani
bila kuelezwa!! Wakati mwingine tunatoa maoni tu kwa uzoefu lakini
kuachwa kwa Maguli hebu kamuulize kocha sasaivi”, llisema Poppe kwa
ukali.
0 comments:
Post a Comment