Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Damian Lubuva
akizungumza katika mkutano na vyama vya siasa kujadili masuala
mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka
huu.
Mkurugenzi wa uchaguzi, Kailima Ramadhan akizungumza na wadau wa vyama vya siasa leo jiji ni Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia maada leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MWENYEKITI
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu ,Damian Lubuva
amevitaka vyama vya siasa kupeleka malalamiko yao katika kamati ya
maadili ya NEC na sio kwenda kutoa malalamiko yao katika vyombo vya
habari.
Lubuva
aliyasema hayo leo wakati NEC ilipokutana na vyama vya siasa kujadili
masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba
25 mwaka huu,amesema kuwa nafasi vya siasa vina nafasi ya kuhamasisha
watu wapige kura kwa wale wenye sifa.
Amesema
wakati wa kupiga kura watu wakipiga kura wanatakiwa kuondoka na kazi
zingine zitafanywa na mawakala ndio watakaofanya kazi zoezi la kuhesabu
na baadae kubandika.
Lubuva amesema watu wakikaa vituoni wanaweza kuvuruga amani na kufanya zoezi la upigaji kura kuharibika.
Amesema tume imejipanga katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru na haki kutokana na mfumo wa kisasa.
Aidha
amevitaka vyama vya siasa kunadi sera zao na sio kushughulika na watu
kwani wananchi wanahitaji sera waweze kufanya maamuzi ya kuchagua
kiongozi.
Baadhi
ya vyama vya siasa vimeridhishwa na ushirikishwaji wa NEC katika
masuala kuelekea uchaguzi mkuu na jinsi walivyojipanga uendeshashaji wa
uchaguzi mkuu.
0 comments:
Post a Comment