https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    UMOJA WA ULAYA KUDHIBITI BOTI ZINAZOVYUSHA WAHAMIAJI

    Umoja wa Ulaya unaanza operesheni mpya za kudhibiti boti zinazovusha wahamiaji kimagendo kukatiza bahari ya Mediterranean.

    Chini ya Operesheni hiyo iitwayo Sophia, boti za vikosi vya wanamaji zitaruhusiwa kuingia, kufanya upekuzi, kuzikamata na kuzitimua boti zinazohisiwa kubeba wahamiaji.

    Hadi sasa Umoja wa Ulaya umejikita katika uangalizi na operesheni za uokoaji wahamiaji ambao boti zao huzama mara kwa mara kutokana na kuwa duni na zenye kujaza mno watu.

    Takwimu zinaonyesha zaidi ya wahamiaji na wakimbizi 130,000 wamekatiza Ulaya wakitokea pwani ya kaskazini mwa Afrika, huku wengine zaidi ya 2,700 wakifa maji.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UMOJA WA ULAYA KUDHIBITI BOTI ZINAZOVYUSHA WAHAMIAJI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top