Kumekuwa
na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya
Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyoripotiwa hivi
karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru. Taarifa hizo
zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake ya Bandari ya Dar es
salaam hivi karibuni.
Uchunguzi
wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa
zilizoingizwa na kampuni hio ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika
katika sakata hilo. Isipokuwa kumetokea upotevu wa makontena
yaliyoingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la
kuhifadhia makontena(ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo la Azam ICD.
Aidha
imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini
TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kampuni hiyo (SSB Group of
Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika na upotevu huo
wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote
wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.
SSB Group of Companies
Corporate Affairs Department
November 29, 2015
CHANZO MICHUZI BLOG
CHANZO MICHUZI BLOG
0 comments:
Post a Comment