Ikiwa
bado siku moja Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe
Magufuli atimize mwezi mmoja toka aapishwe kuwa Rais wa awamu ya tano wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeshuhudia mengi yakitokea katika
suala zima la upambanaji na watu wanaokwepa kodi sambamba na
kusimamishwa kazi kwa viongozi kadhaa wa mamlaka ya mapato Tanzania
(TRA) waliopo Bandarini.
December
4 kasi ya Rais John Pombe Magufuli inaonekana kuwashitua viongozi wa
mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), kwani wameanza harakati za kuwaadhibu
watu wanaodaiwa kodi.
Juma
lililopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liliaga timu ya
Taifa ya Vijana Chini ya umri wa miaka 15 (U15) ikianza ziara yake ya
Afrika Mashariki kuanza kucheza na Burundi mjini Kigoma na baadaye
Kigali, Rwanda, Kampala, Uganda na mwisho Nairobi Kenya.
Bahati
mbaya ziara hiyo itaishia Mwanza na Kigoma kufuatia Mamlaka ya Mapato
Tanzani (TRA) kuizuia account ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania
(TFF) kwa kushindwa kulipa kodi ya Tsh bilioni 1,637,334,000 (bilioni
1.6 tshs) ikiwa ni kodi kwa kipindi cha 2010 – 2013
Sehemu
kubwa ya kodi hiyo ni makato kwenye mishahara (PAYE) ya walimu wa
kigeni, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Jacob Michelsen na vilevile kodi ya
ongezeko la thamani (VAT) kwenye mchezo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars)
dhidi ya Brazili uliofanyika mwaka 2010.
Walimu
wa Timu za Taifa wamekuwa wakilipiwa mishahara na Serikali na hivyo TFF
haikuwajibika kuwakata kodi. Aidha, mchezo kati ya Tanzania na Brazil
ulisimamiwa na kamati maalum ya Serikali na fedha zake hazikuingizwa
katika akaunti za TFF.
Kutokana na hatua hii ya TRA shughuli nyingine za mpira zitakazohathirika ni:
1.
Kulipia madeni ya usafiri, chakula na posho za Timu za Taifa
zilizoshiriki mtoano wa kombe la Dunia na mashindano ya Afrika Mashariki
na Kati (Challenge Cup)
2. Program za mpira wa Wanawake na vijana zitalazimika kusimama.
3. Mashindano ya kombe la Shirikisho raundi ya pili iko kwenye hatihati kwani hakuna fedha za kugharimia michezo hiyo.
4.
Mashindano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoendelea yatalazimika
kusimama vilevile. Mashindano haya TFF imekuwa ikiyaendesha bila
mdhamini.
5.
Vifaa vya michezo (Mipira) kwa ajili ya shule za msingi na vituo vya
maendeleo (Regional Football Development Centres) vinatarajiwa kuwasili
nchini wakati wowote na TFF haitakuwa na uwezo wa kulipia usafirishaji
na ushuru wake.
6.
Malipo ya gharama za kambi na karo kwa ajili ya vijana wa timu ya Taifa
ya vijana chini ya miaka 13 walioko shule ya Alliance Academy ya jijini
Mwanza.
7.
Huduma za kiutawala ikiwa ni pamoja na utunzaji viwanja na majengo,
maji, umeme, ulinzi pamoja na mishahara na stahiki nyingine za
wafanyakazi
8.
Mwelekeo na mwitikio mzuri wa wadhamini uko kwenye hatari ya kupotea
pindi mashindano na shughuli wanazozidhamini zitakapofubaa au kusimama
kabisa.
9.
Mkutano Mkuu wa kawaida wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wa Mwaka
2015 uliopangwa kufanyika Tanga 19-20 Desemba 2015 sasa una hatihati ya
kuweza kufanyika.
Hata
hivyo, kwa kutambua umuhimu wa ulipaji kodi na wajibu wa Mamlaka ya
Mapato katika kuhakikisha kodi inakusanywa kwa ajili ya ustawi na
maendeleo ya Taifa,TFF ipo katika mawasiliano na TRA katika kutafuta
ufumbuzi wa kudumu wa suala hili ikiwa ni pamoja na kupitia upya
mahesabu ili kujua wajibu halisi (net liability) wa TFF na namna ya
kulipa au kulipwa kutegemea ulali wa mahesabu.
Kwa
taarifa hii TFF inaomba utulivu kwa wanamichezo wote pamoja na
ushirikiano wa karibu kutoka katika vyombo vyote husika ikiwemo TRA na
wadau wengine ili jambo hili lipate ufumbuzi wa kudumu utakaoleta tija
kwa serikali ya awamu ya tano ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji
katika maendeleo ya mpira wa miguu na michezo kwa ujumla wake.
0 comments:
Post a Comment