Ikiwa bado siku moja Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli atimize
mwezi mmoja toka aapishwe kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, tumeshuhudia mengi yakitokea katika suala zima la
upambanaji na watu wanaokwepa kodi sambamba na kusimamishwa kazi kwa
viongozi kadhaa wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) waliopo Bandarini.
December 4 kasi ya Rais John Pombe
Magufuli inaonekana kuwashitua viongozi wa mamlaka ya mapato Tanzania
TRA kwani wameanza harakati za kuwaadhibu watu wanaodaiwa kodi, November
4 stori za kuaminika kutoka TRA ambazo zimeripotiwa n muhandishi wa
habari za michezo Shaffih Dauda, zinatajwa kuizuia account ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa kushindwa kulipa kodi ya Tsh bilioni 1.6.
Kitendo cha mamlaka ya mapato Tanzania
(TRA) kuizuia account ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) kinatajwa ni
kasi ya Rais mpya wa awamu ya tano ambaye kwa kipindi hiki anaonekana
kusimamia kila shilingi inayotoka na kuingia mahali fulani iwe imefuata
utaratibu fulani sambamba na kuilipia kodi.
Msisitizo wake mkubwa Rais Magufuli katika suala la kodi ili wananchi wapate huduma
“Kwa wale ambao bahati mbaya walikwepa kulipa kodi na wakayapitisha
makontena, wasihangaike kuyafichaficha natoa siku saba tu wakalipe kodi
halafu wakaishi kwa raha, kontena sio kama sindano ukilibeba mwishowe
litakuponda bure“
Kama ulipitwa na msisitizo wa Rais Magufuli kuhusu kodi alivyoongea na wafanyabiashara kuhusu kodi video yake hii hapa
0 comments:
Post a Comment