Kuna msanii mmoja wa muziki wa kizazi kipya anafahamika kwa jina la Afande Sele kutoka kundi la Watupori kutoka mkoani Morogoro alishawahi kutamba na wimbo mmoja unaoitwa ‘Dunia inamambo’, sasa kweli naamini dunia inamambo baada ya watu kukaa chini na kuifananisha safu ya serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Mgufuli na safu ya ushambuliaji ya Barcelona inayoongozwa na Lionel Messi ambayo inatazamwa kuwa ndiyo safu ya ushambuliaji tishio kwa sasa duniani.
Safu ya mtu tatu inayoongozwa na Rais Magufuli inakamilishwa na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Balozi Ombeni Sefue.
Tangu serilikali ya awamu ya tano iikaningie madarakani kumekuwa na hali ya ‘mshikemshike’ na ziara za kushtukiza za mara kwa mara zinazofanywa na viongozi hao ambao wakikuta mambo hayaendi sawa basi lazima vumbi litimke kwa wahusika ikiwa ni pamoja na watu kutimuliwa kazi, kusimamishwa kazi na wengine kuwekwa ndani.
Utendaji huu wa kazi wa serikali hii ambayo imeingia madarakani October 25, 2015 umejizolea sifa kemkem hadi sasa na hii ndiyo sababu kubwa ambayo hadi sasa erikali hiyo inayoongozwa na mtu tatu inafananishwa na ile combination ya ushambuliaji ya Barcelona ya Messi, Neymar na Suarez ambayo imekua hatari kwa mabeki wa timu pinzani kutokana na kupasia kwao kamba.
Safu hizo zimefananishwa kama ifuatavyo; Magufuli=Messi, Majaliwa=Neymar na Sefue=Suarezi, je wewe unaona hii imekaaje, nani kapewa nafasi ambayo siyo yake hapo?
Ukitaka kuhakikisha kwamba safu ya ushambuliaji ya Barcelona ni balaa wala usipate tabu sana, siku chache zilizopita FIFA ilitangaza wachezaji ambao wameingia fainali ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2015, wachezaji wawili kati ya watatu wanaounda safu hii ya ushambuliaji wameingia kwenye fainali ya kinyang’anyiro hicho. Hawa si wengine bali ni Lionel Messi na Neymar wote wakitoka kwenye timu ya Barcelona pia kwenye safu ya ushambuliaji inayotishia zaidi usalama wa mabeki.
Mtandao huu unaungana na watandania wengie wapenda maendeleo kuipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli akishirikiana na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa pamoja Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue hakika haya ni majembe na tunaiona kauli mbiu yao ya #Hapa Kazi Tu ikitekelezwa, Hongereni sana.
0 comments:
Post a Comment