Japo headlines za siasa zilionekana
kubeba uzito mkubwa miezi michache iliyopita, bado kuna mengine
yaliendelea kwenye upande mwingine ikiwemo ishu ya ugonjwa wa
kipindupindu ambao umeendelea kuripotiwa kwenye mikoa mbalimbali
Tanzania.
Ripoti iliyonifikia leo inaonesha idadi
ya wagonjwa waliougua kipindupindu mpaka sasa ni watu 10,412 huku ripoti
ikionesha wengine 159 kuwa wamefariki baada ya kuugua… bado
kipindupindu kipo, wagonjwa 97 bado wamelazwa katika maeneo mbalimbali.
Taarifa ya habari kituo cha ITV imesema maeneo yanayoongoza kuwa na wagonjwa wengi kwa sasa ni Kyela Mbeya ambako kuna wagonjwa 34, Arusha Mjini wagonjwa 11 na Ilemela Mwanza kuna wagonjwa 7.
Taarifa yote ya Habari ITV hii hapa ikiwa na ripoti yote.
0 comments:
Post a Comment