Watu wanne wamefariki na wengine wawili wamelazwa katika kituo cha afya cha kifula wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo katika wilaya hiyo juzi na jana na kusababisha mafuriko na mmomonyoko wa miamba.
Mkuu wa wilaya hiyo Bw Shayibu Ndemanga amesema, watu wawili
waliokuwa wamepakia bodaboda walisombwa na maji katika daraja la mto
Makokoro walipokuwa wakivuka ambapo kamati ya ulinzi na usalama pamoja
na kushiriki usafi lakini walikwenda kutafuta miili ya marehemu kando ya
mto huo bila mafanikio.
Bw Ndemanga ameiambia ITV kuwa watu wengine wawili walifariki baada
ya kusombwa na maji na kutumbukia bwawa la nyumba na mtoto kuangukiwa
na miamba ya mawe kwenye nyumba aliyokuwa amelala katika kijiji cha
Vuaga na wengine wawili kulazwa kituo cha afya cha Kifula tarafa ya
Ugweno.
Mkazi wa mji wa Mwanga Bw Kajiru Mfanga ameiomba serikali ijenge
daraja kubwa katika mto huo na kuongeza idadi ya makaravati ambayo
yatasaidia kudhibiti wingi wa maji yanayotiririka kutoka milima ya
Usangi na Ugweni.
0 comments:
Post a Comment