Najua nina watu wangu wao na selfie
damdam, taarifa ikufikie kwamba kuna maeneo imebidi selfie zipigwe
marufuku kwa ajili tu ya usalama wa watu.
Sababu ya Serikali kuamua kuingia kati
na kuzuia selfie ni ishu za ajali zinazosababisha vifo, kuna ajali
ambazo India wanazo kwenye record zao !! Iko ishu ya ajali ya mtalii
mmoja kufariki baada ya kuteleza kwenye ngazi za makumbusho ya Taj Mahal, India alipokuwa akijipiga selfie.
Iko pia stori ya wasichana wawili
walioanguka baharini kutoka kwenye ukuta wa ukingo wa bahari wakijipiga
selfie, mmoja akafariki mwingine akatoka salama… Jeshi la Polisi limeona
kuna kila sababu wakasogea hatua moja kwa kutangaza maeneo 15 ambayo ni
hatari na ni marufuku kupiga selfie..
Sehemu kubwa ya maeneo ambayo ni marufuku kupiga selfie kwa Mumbai India, ni maeneo ambayo yanatembelewa na ni kivutio kikubwa cha watalii wengi.
Kingine ni kwamba kuna mpango wa kuwekwa pia mabango yaliyoandikwa ‘No Selfie Zone‘
Story ya ajali ya wasichana waliotumbukia kwenye maji wakati wakijipiga selfie
0 comments:
Post a Comment