https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Guardiola au Pellegrini: Nani Ataingia kwenye listi hii ya makocha waliondoka kwenye vilabu vyao na ushindi wa Kombe la ulaya

    PEP GUARDIOLA anaweza kuingia kwenye rekodi ya kocha wa 11 kumaliza utawala wake katika klabu moja kwa kushinda kombe la ulaya ikiwa tu Bayern Munich watafanikiwa kutwaa ubingwa wa Champions League msimu huu.
    Mhispania huyo atahamia Manchester City mwishoni mwa msimu huu – na anaweza kufanikiwa kuondoka Bayern na heshima kubwa kwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mikubwa zaidi barani ulaya ngazi ya klabu.
    Jambo hilo pia linaweza kutokea kwa kocha, Manuel Pellegrini. 02_03153555_75ce34_2671531aWakati SunSport looks back at the ten managers who left their clubs on the ultimate high.


    Jose Villalonga, Real Madrid: 1957

    Kocha mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushinda kombe hili – miaka 36. 

    Alishinda ubingwa wa ulaya mara mbili – kabla ya kwenda kuiongoza Spain katika Euro 1964.
    Villalonga aliondoka Real kwa mafanikio na aliiacha ikiwa kwenye hali nzuri kwa sababu walienda kushinda makombe ya michuano mitatu iliyofuatia.


    Luis Carniglia, Real Madrid: 1959

    Inawezekana ilikuwa rahisi kuwa kocha wa Real Madrid wakati huo.


    Kocha wa huyo wa Kiargentina alifanikiwa kurithi vizuri mikoba ya Villalonga.
    Aligundulika kuwa na ugonjwa wa figo na akaamua kuacha kazi kufuatia ushindi dhidi ya Stade Reims.



    Bela Guttman, Benfica: 1962

    03_03153555_9800cf_2671533aMshindi mwingine wa kombe la ulaya – ingawa aliondoka kwa akiwa hana maelewano mazuri na uongozi. 
    Kocha huyu kutoka Hungary aliomba kuongezewa mshahara, uongozi ukamkatalia. Baada ya hapo Guttman akatoa maneno mazito akisema kwamba ‘Benfica hatiweza kushinda ubingwa wa ulaya tena.’
    Kabla ya fainali ya mwaka 1990 kati ya Benfica vs AC Milan huko Austria, ambapo Guttman alizikwa, huku akitokwa na machozi gwiji wa Benfica Eusebio alipiga magoti kwenye kaburi la Guttman na kumuomba aisamehe klabu yake na kuondoa kauli yake ya laana kwa Benfica.
    Hata hivyo, mpaka leo tangu Guttman alipoondoka – Benfica wamecheza fainali 8 za ulaya na hawajaahi kutwaa kombe lolote la ulaya.


    Nereo Rocco, AC Milan: 1963

    04_03153555_a37620_2671534aMuanzishilishi wa mfumo wa ‘catenaccio’ — mfumo ambao ulileta mafanikio makubwa katika soka nchini Italia.

    Rocco alioongoza Rossoneri kushinda dhidi ya Benfica, lakini akaondoka na kwenda kuifundisha Torino.
    Akarejea tena Milan miaka minne baadae na kushinda ubingwa mwingne wa ulaya mnamo mwaka 1969.


    Rinus Michels, Ajax: 1971

    05_03153555_564b13_2671535aKutoka kwa mgunduzi wa mfumo bora wa ulinzi mpaka kwa mtalaamu wa soka la mfumo wa Total Football.
    Michels alitengeneza mfumo ambao ulikuwa mgeni machoni mwa watu wa kushambulia wakati wadachi hao walipoifunga Panathinaikos.
    Pia aliiongoza Uholanzi katika fainali za kombe la dunia mwaka 1974, kabla ya kuipa ubingwa pekee wa kimataifa wa ulaya wakati aliporejea kuifundisha tena timu hiyo mwaka 1988.


    Emeric Ienei, Steaua Bucharest: 1986

    06_03153555_c775e6_2671537aAnawakilisha mafanikio makubwa pekee katika historia ya soka la Romania.

    Steaua Bucharest iliustua ulimwengu wa soka wakati walipoifunga Barcelona na kushinda ubingwa wa ulaya. Wakatalunya walikuwa wakifundishwa na kocha wa kiingereza Terry Venables.


    Raymond Goethals, Marseille: 1993

    07_03153555_4046d1_2671539aKocha wa huyu Kibelgiji ana historia ya kuwa kocha wa kwanza kushinda kombe la  Champions League.
    Alifanikiwa kupata mafanikio haya akiwa na umri na miaka 72 – kocha mwenye umri mkubwa zaidi kushinda kombe hilo.
    Wengi wanaomjua wanasema aliondoka wakati sahihi kwa mafanikio.
    Baada ya kuondoka kwa kocha huyo mambo yakawa tofauti upande wa Marseille, ambao walishuka daraja kutoka Ligue 1 kwa makosa ya kupanga matokeo na hawakuruhusiwa kuutetea ubingwa wao.


    Ottmar Hitzfeld, Borussia Dortmund: 1997

    08_03153555_294a13_2671540aMjerumani huyu alishinda ubingwa wake kwanza wa ulaya akiwa na timu hiyo inayovaa jezi za njano na nyeusi.

    Dortmund walikuwa wanajitengenezea jina katikati mwa miaka ya 90.
    Ilikuwa jambo la kushtua wakati walipoifunga Juventus waliokuwa mabingwa watetezi jijini Munich mwaka 1998.


    Jupp Heynckes, Real Madrid: 1998

    09_03153555_0ff47b_2671541aKocha pekee kwenye listi hii ambaye aliondoka kwa kufukuzwa.

    Aliambiwa aondoke baada ya kuiongoza Real Madrid kushinda ubingwa wa kwanza wa ulaya mwaka 1966.
    Heynckes alikuwa na wastani m’baya wa matokeo kwenye ligi, na hilo lilipelekea kufukuzwa kwake.


    Jose Mourinho, Porto: 2004

    10_03153555_e89b97_2671542aSPECIAL ONE alijitengeneza jina barani ulaya.
    Alianza kwa kushindwa ubingwa wa ligi, kombe la FA ya Ureno na UEFA Cup na kisha msimu uliofuatia akashinda Champions League.
    Kabla hajaondoka na kuhamia Chelsea.


    Jose Mourinho, Inter: 2010

    11_03153555_be71f9_2671543aMourinho alishinda makombe matatu ndani ya msimu mmoja na Inter Milan – mojawapo ya makombe hayo ilikuwa kombe la kwanza la ulaya baada ya miaka 45.
    Na baada ya hapo akahamia Santiago Bernabeu.


    Jupp Heynckes, Bayern Munich: 2013

    12_03153555_d27f6e_2671544aMashabiki wa CITY angalieni hili.
    Heynckes aliambiwa mwezi January kwamba Guardiola angemrithi mwishoni mwa msimu.
    Lakini hilo halikumpotezea umakini kwa sababu aliiongoza Bayern kwenda kushinda makombe matatu kwa mara ya kwanza katika historia ya soka la Ujerumani.
    Inawezekana labda hili nalo likamtokea  Pellegrini?
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Guardiola au Pellegrini: Nani Ataingia kwenye listi hii ya makocha waliondoka kwenye vilabu vyao na ushindi wa Kombe la ulaya Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top