Mwanafilosophia
na mwanauchumi Eric Thomas aliwahi kutoa kauli yake moja maarufu
(quote) akisema “winners focus on winning, losers focus on winners”
akimaanisha washindi wanazingatia kwenye ushindi na washindwa
wanazingatia kuwaangalia washindi.
Nimeukumbuka
usemi huu baada ya kuingalia timu ya Arsenal kwa miaka 10 ya karibuni
baada ya kuondoka vizazi vya akina Viera, Eeaman, Tony Adams, Thierry
Henry na wengineo kibao. Imekuwa ni timu yenye kushindwa kumaliza vizuri
karata zake ikiwemo karata ya ubingwa wa ligi kuu na karata ya ubingwa
wa klabu bingwa Ulaya.
Matukio
kama haya yana sababu nyingi za kisoka ikiwemo sera (philosophy)
mbalimbali za mzee wenger, mtisho wa kikosi(squad pressure) na ndiyo
maana ni jambo la kawaida kumuona Oliver Giroud, Flamin, Sanogo, na hata
Aarteta kila alfajiri wanapaki magari yao ya thamani pale London kwa
ajili ya mazoezi wakati Payet, Mahrez, Lukaku wakiwa sehemu zingine.
Anguko
la mzee Wenger lina sababu nyingi ikiwemo bajeti ya klabu kutokana na
ujenzi wa uwanja wao wa Emirates, lakini binafsi moja ya sababu ya
anguko la mzee wenger ni kuanza kuiga na kuwaangalia wanaofanya vizuri
pasipo kuwa na uhakika na anachokifanya.
Mzee
wenger aliamua kuwaiga FC Barcelona kutumia vipaji vya shule yao ya
soka ya La Masia na yeye kuamua kuanza kutegemea wachezaji makinda
kutoka kwenye academy yake na wengine kuwanunua, na kuamua kuwaacha
akina Kolo Toure, Emanuel Adebayor, Reyes, Eboue na wengine kibao na
kuanza kuwapa nafasi akina Cesc Fabrigas, Jack Wilshere na akina Gibbs.
Sahau
mfumo wa kuiga academy bado akilini mwa mzee wenger anaamini maadui
zake wakubwa wa mafanikio ni akina Manchester United, Liverpool na
Chelsea na kusahau kuna akina Man City, Tottenham, na Leicester city.
Sehemu
ambayo Wenger anaweza akawa shahidi mzuri wa maneno ya Eric Thomas ni
kitendo chake cha kuamua kumuiba na kumpa mkataba muibua vipaji (scout)
wa timu ya Leicester City na kusahau mafanikio ya Leicester City msimu
huu yana sababu nyingi za kisoka mbali na na muibua vipaji huyo.
Usiku
wa Jumatano ya tarehe 16/03/2016 nchini Spain katika jiji la Barcelona,
mzee Wenger atakwenda kutaka kufanya jaribio la kupindua matokeo mbele
ya timu yenye washambuliaji watatu wenye thamani ya pound Mil 500
(Lionel Messi 250,Neymar 150 na Suarez 100) dhidi ya timu ya
washambuliaji wenye thamani ya pound Mil 130 (Mesut Ozil 65, Alex
Sanchez 50 na Oliver Giroud 20).
Binafsi
naamini mzee wenger atakuwa Nou Camp kama shahidi wa maneno ya Eric
Thomas na siyo kama mpingaji wa maneno hayo. Mzee Wenger na koti lake
maridadi atakwenda kuwa kama muangaliaji wa mafanikio ya wanaofanikiwa
na siyo mpiganaji wa mafanikio yake. Kila la kheri The Gunners kwenye
usiku wa Ulaya.


0 comments:
Post a Comment