Tumeshazoea sana kuwaona wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil wakiwa
wamevaa jezi zao za kijani na njano na wengine huhisi labda wamekuwa
wakivaa jezi za rangi hiyo kwa miaka yote, wakati ukweli ni kwamba
Brazil walibadilisha kutoka rangi nyingine kuja kwenye rangi za sasa.

Brazil walikuwa wakitumia jezi nyeupe full mpaka katika fainali ya kombe la dunia 1950 ambayo walikuwa wenyeji wa michuano. Walifika fainali na wakafungwa na Uruguay katika uwanja wao maarufu wa Maracanazo na baada ya hapo shirikisho la soka la nchi hiyo likaamua kubadilisha rangi za jezi, katika jaribio la kufuta kabisa za aibu ya kufungwa nyumbani tena kwenye fainali ya kombe la dunia – fainali ambayo ilimtia doa jeusi golikipa Moacie Barbosa na maisha yake yote ya soka ndani ya nchi ya wapenda soka.
Brazil
wakahamia kwenye jezi za bluu – na bahati mbaya ikaendelea kuwa upande
wao – wakaondolewa kwenye Copa America jijini Kima kwa kufungwa na
Paraguay.
Baada ya hapo, gazeti maarufu la nchi hiyo Correio da Manhá likaandaa shindano, la kuwaambia mashabiki kutengeneza mawazo mapya ya utengezaji wa jezi mpya lakini lazima wahusishe rangi kutoka kwenye bendera ya nchi yao: Njano, kijani, bluu na nyeupe. Mmoja ya watu aliyekuja na mawazo alikuwa ni mbunifu wa michoro ambaye pia alitengeneza mchoro rasmi wa michuano ya kombe la dunia 1950, lakini wazo lake la jezi zenye rangi 3 – tshirt ya kijani, soksi nyeupe na bukta za blue, lilikataliwa.
Mshindi alikuwa kijana wa miaka 19, ambaye alikuwa mchoraji akifanya
kazi katika gazeti moja kusini mwa Brazil, aliyefahamika kama Aldyr
Garcia Schlee. Ubunifu wake wa kutengeneza jezi za njano juu, zilizo na
mstari na wa kijani kwenye kora na mikononi, bukta ya blue na soksi
nyeupe – lilipitishwa na wengi. Brazil wakaanza rasmi kuzitumia jezi
hizo katika mechi vs Chile na kwa bahati nzuri wakaanza na ushindi mnamo
usiku wa kuamkia 15 March, 1954.
Brazil waliendelea na jezi zao mpya kwenye michuano ya kombe la dunia huko Switzerland mwaka 1954 lakini wakaishia kutolewa na Hungary katika mechi iliyopewa jina la ‘Battle of Berne’. Lakini kwa wakati huo, Hungary walikuwa wakifahamika kuwa miongoni mwa timu bora duniani jambo lilipelekea aibu miongoni mwa wabrazil kutokuwa kubwa.
Hatimaye
Brazil wakashinda ubingwa wa dunia katika michuano iliyofuatia, lakini
wakiwa wanatumia jezi zao za bahati za njano – kasoro kwenye fainali tu,
ambayo walicheza na Sweden – ambao ndio walikuwa wenyeji wa michuano na
hivyo walikuwa wanavaa jezi zao za njano na ikawalazimu Brazil kuvaa
jezi zao blue. Tangu wakati the Seleção wameshinda kombe la dunia mara
nyingi kuliko nchi yoyote na ndio timu pekee ambayo ina rekodi ya
kucheza kila michuano ya kombe hilo tangu ilipoanzishwa mwaka 1930.
Brazil walikuwa wakitumia jezi nyeupe full mpaka katika fainali ya kombe la dunia 1950 ambayo walikuwa wenyeji wa michuano. Walifika fainali na wakafungwa na Uruguay katika uwanja wao maarufu wa Maracanazo na baada ya hapo shirikisho la soka la nchi hiyo likaamua kubadilisha rangi za jezi, katika jaribio la kufuta kabisa za aibu ya kufungwa nyumbani tena kwenye fainali ya kombe la dunia – fainali ambayo ilimtia doa jeusi golikipa Moacie Barbosa na maisha yake yote ya soka ndani ya nchi ya wapenda soka.
Baada ya hapo, gazeti maarufu la nchi hiyo Correio da Manhá likaandaa shindano, la kuwaambia mashabiki kutengeneza mawazo mapya ya utengezaji wa jezi mpya lakini lazima wahusishe rangi kutoka kwenye bendera ya nchi yao: Njano, kijani, bluu na nyeupe. Mmoja ya watu aliyekuja na mawazo alikuwa ni mbunifu wa michoro ambaye pia alitengeneza mchoro rasmi wa michuano ya kombe la dunia 1950, lakini wazo lake la jezi zenye rangi 3 – tshirt ya kijani, soksi nyeupe na bukta za blue, lilikataliwa.
Brazil waliendelea na jezi zao mpya kwenye michuano ya kombe la dunia huko Switzerland mwaka 1954 lakini wakaishia kutolewa na Hungary katika mechi iliyopewa jina la ‘Battle of Berne’. Lakini kwa wakati huo, Hungary walikuwa wakifahamika kuwa miongoni mwa timu bora duniani jambo lilipelekea aibu miongoni mwa wabrazil kutokuwa kubwa.

0 comments:
Post a Comment