Matumaini ya Manchester City ya kutwaa kombe la Ligi Kuu ya Uingereza yamekabiliwa na kizingiti baada ya kutoka sare tasa na timu iliyomkiani ya Norwich na kuishia kuwa nyuma kwa pointi tisa dhidi ya vianara Leicester huku ikibakia michezo tisa tu.
Kipa wa Norwich John Ruddy alidhibiti michomo ya Sergio Aguero isitinge wavuni, huku wenyeji hao wakifanikiwa kuwanyima ushindi muhimu wageni Manchester City.
Sergio Aguero akidhibitiwa asilete madhara kwenye goli la Norwich
Katika mchezo mwingine Graziano Pelle alifunga mara mbili na kuifanya Southampton kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stoke City. Pia Bournemouth 3-2 Swansea.
Muitalia Pelle, ambaye hajawahi kufunga katika michezo 12, alifunga mara mbili katika kipindi cha kwanza kwa kupitia kichwa cha kuparaza na la pili kwa shuti la chini.
Pelle akiruka juu na kuupiga kichwa cha kuparaza mpira uliojaa wavuni

0 comments:
Post a Comment