

Takwimu muhimu unazotakiwa kuzifahamu

- Simba wameshinda mchezo wa tatu mfululizo baada ya kufungwa na Yanga bao 2-0. Imeshinda 2-0 dhidi ya Mbeya City, ikaifunga 3-0 Ndanda FC kabla ya leo kuilaza Tanzania Prisons kwa bao 1-0.
- Jackson Mayanja amefanikiwa kupata ushindi wake wa 9 katika mechi 10 ambazo amesimama kama kocha akikiongoza kikosi cha Simba baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Dylan Kerr.

- Timu zote zimepata ushindi kwenye michezo yake ya nyumbani msimu huu. TZ Prisons waliifunga Simba kwa bao 1-0 kwenye uwanja wao Sokoine, Mbeya. Simba nao wamepata ushindi kama huo kwenye uwanja wanaoutumia kama uwanja wao wa nyumbani.

- Simba wamefunga magoli kuanzia dakika ya 70 na kuendelea kwenye mechi mbili mfululizo. walifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City na leo dhidi ya Tanzania Prisons.
Michezo mingine iliyochezwa March 13 kwenye viwanja vingine matokeo yake yapo kama ifuatavyo.
Majimaji 1-0 Stand United
Kagera Sugar 3-0 Coastal Union
Mgambo JKT 1-1 Mwadui FC


0 comments:
Post a Comment