https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    SPIKA AKUTANA NA WABUNGE KUTOKA UJERUMANI


    dg1
    Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimkabidhi zawadi Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Jens Koeppen. Anayeshuhudia kulia ni Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson.Wabunge hao walimtembelea Spika ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam
    dg2
    dg3
    Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akipokea zawadi Kutoka kwa Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Jens Koeppen. Wabunge hao walimtembelea Spika ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam
    dg4
    Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Kiongozi wa Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Jens Koeppen (wa pili kushoto) waliomtembelea Spika ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson na wa Kwanza kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini Bw. Egon Kochake.
    dg5
    Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiagana na Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Jens Koeppen waliomtembelea Spika ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia wa kwanza kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson na wa Kwanza kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini Bw. Egon Kochake.
    dg6
    Spika wa Bunge (wa pili kutoka kulia kwa walio kaa) akiwa katika picha ya Pamoja na Wabunge la Ujerumani waliomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson, Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Jens Koeppen na Balozi wa Ujerumani nchini Bw. Egon Kochake.
    (Picha na Ofisi ya Bunge)

    DC GEITA:TAMASHA LA PASAKA NI JAMBO KUBWA KWETU

    download (3)
    Na Mwandishi Wetu
    MKUU wa Wilaya ya Geita Manzie Mangochie anasema  Tamasha la Pasaka ni jambo kubwa sana kwao kwa sababu linafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.
    Mangochie anasema ukubwa na umuhimu wa tamasha hilo ni kutajwa kwa neno la Mungu na waimbaji sambamba na viongozi mbalimbali wa dini wanaofika katika tamasha hilo.
    Mangochie anasema Mkoa wa Geita una matatizo mengi  ambayo yalikuwa yanahitaji kukemewa, lakini mwaka huu Mungu amesikia matakwa ya wakazi wengi wa mikoa hiyo ambayo ilitawaliwa na matukio ya mauaji yakiwemo ya vikongwe  na walemavu wa ngozi ‘Albino’.
    “Mikoa hii ya Kanda ya ziwa iligubikwa na shetani ambaye ni mauaji ya Maalbino na Wakongwe ambao walikuwa wakitendewa unyama ambao Mungu alikuwa akichukizwa nao, hivyo kupitia Tamasha la Pasaka neno la Mungu litasaidia kuondosha madhila hayo,” alisema Mangochie.
    Mangochie anasema kupitia Tamasha la Pasaka waandaaji watasaidia wakazi wa mikoa hiyo kuachana na kusahau matukio ya kumchukiza Mungu.
    Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanaendelea vilivyo kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.
    Msama alisema tamasha hilo linatarajia kuanza Machi 26 kwenye ukumbi wa Desire ulioko mkoani Geita, Machi 27 litafanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na Machi 28 litafanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.
    Msama alisema viingilio kwa wakubwa ni shilingi 5000 na watoto shilingi 2000 ambako alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SPIKA AKUTANA NA WABUNGE KUTOKA UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top