WAYNE ROONEY kwa mara nyingine ameendelea kuliandika jina lake kwenye vitabu vya historia ya soka baada ya usiku wa kuamkia leo kufunga goli katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya England dhidi ya Bournemouth.
Rooney alifunga goli la kwanza la ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Bournemouth katika dimba la Old Trafford – na goli hilo limemuingiza katika rekodi ya kuwa mchezaji wa pili katika historia ya EPL kufunga magoli 100 au zaidi katika uwanja mmoja Uingereza – Rooney akitimiza magoli 100 katika dimba la Old Trafford.
Thierry Henry ndio mchezaji mwingine pekee ambaye amefunga magoli zaidi ya 100 katika uwanja mmoja – amefunga magoli 114 katika uwanja wa Highbury.
Goli la kwanza la Rooney ndani ya Old Trafford ilikuwa dhidi ya mechi maarufu ya ‘Pizzagate’ dhidi ya Arsenal ambaho United walishinda 2-0 mnamo mwaka 2004.
Nahodha huyo wa England na Manchester United sasa anahitaji magoli manne tu ili kuifikia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote wa Manchester United ya Bobby Charlton ambaye aliifungia United magoli 249, Rooney mpaka sasa ana magoli 245.
0 comments:
Post a Comment