Afisa
Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Ilse Boshoff na Mkurugenzi wa Masoko
na Mawasiliano wa kapuni hiyo Allan Chonjo (kulia) wakizindua chapa
mpya ya saruji iitwayo “Tembo Fundi” ambayo ni mahususi kwa ajili ya
uashi leo kwenye kiwanda cha Saruji cha Tembo Cement jijini Mbeya
(Picha: Mpiga Picha Wetu).
Mkurugenzi
wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (kushoto),
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Ilse Boshoff (katikati) na Emily
Sindato (kulia), Mkuu wa Ufundi wa kiwanda hicho wakizindua chapa mpya
ya saruji iitwayo “Tembo Fundi” ambayo ni mahususi kwa ajili ya uashi
leo kwenye kiwanda cha Saruji cha Tembo Cement jijini Mbeya.
(Picha: Mpiga Picha Wetu)
(Picha: Mpiga Picha Wetu)
Kampuni
ya Saruji Lafarge Tanzania imezindua saruji ya kwanza maalumu kwa
matumizi ya uashi. Saruji hii inayojulikana kama Tembo Fundi itawapa
wajenzi chaguo bora kwa ajili ya kazi za uashi ikiwa ni pamoja na kupiga
plasta ukuta, kusakafia, kujengea tofali na kupangilia marumaru. Saruji
hiyo iliyotengenezwa maalum kwa kazi ya uashi wa kuta za nje na ndani
ina ubora katika kufanya kazi, nguvu kwenye ugundishaji inashika vizuri
na ina umaliziaji bora wenye kuleta matokeo yaliyo bora zaidi kwenye
kujenga tofali, uzio, marumaru na sakafu.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Ilse Boshoff, alisema wakati wa uzinduzi
leo kwamba Tembo Fundi imeundwa mahususi kwa ajili ya kazi za uashi na
kuwapa wajenzi utendaji bora wa kazi na thamani ya fedha.
“Ikiwa
imetengenezwa kutokana na uzoefu na utaalamu wa Lafarge kimataifa
katika kuzalisha saruji, Tembo Fundi ni rahisi kutumia katika kupiga
plasta, tofauti na saruji ya matumizi ya jumla ambayo itamchukua muashi
muda mrefu katika kusawazisha ukuta.
Alisema
faida nyingine muhimu katika matumizi ya Tembo Fundi ni unafuu katika
gharama kutokana na mfuko mmoja wa Tembo Fundi kutumika eneo pana zaidi
ukilinganisha na mfuko wa saruji ya matumizi ya jumla. Kutokana ya
kwamba inafanya kazi vizuri na uimara wake kudumu kwa muda mrefu Tembo
Fundi itawasaidia wajenzi kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge, Allan Chonjo alisema daima
Lafarge imekuwa ikiwasikiliza wateja wake. Tembo Fundi ndio suluhisho la
mahitaji ya saruji yenye ubora kwani inatumia maji kidogo, inadumu,
haipati nyufa na ina uwezo wa kujenga eneo pana zaidi na kuufanya ukuta
wako ung’ae zaidi.
“Tembo
Fundi inapatikana katika ujazo wa kilogramu 50 na ni ubunifu wetu
katika kurahisisha kazi za uashi. Lafarge imewekeza sana katika utafiti
uliopelekea uvumbuzi wa saruji kama hii ambayo inapendwa na wajenzi
katika masoko mbalimbali kimataifa. Hii ni moja ya dhima zetu za
kuhakikisha tunawapa wajenzi sulhisho maalumu katika kazi zao. Tembo
Fundi itasambazwa katika maduka yetu yote ya jumla na rejareja pamoja na
kwenye kontena zetu za usambazaji.
Hivi
sasa kwenye soko la saruji hakuna saruji iliyotengenezwa mahususi kwa
ajili ya uashi jambo ambalo linawalazimisha watumiaji kutumia saruji ya
matumizi ya jumla kwa ajili ya kazi za uashi na kupelekea ongezeko la
gharama za ujenzi na kukosa matokeo mazuri katika ujenzi.




0 comments:
Post a Comment