https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Dalili nyingine ya Zlatan Ibrahimovic kuelekea kujiunga na Man United

    Usiku wa June 9 taarifa za staa wa zamani wa klabu ya Paris Saint Germain yaUfaransa Zlatan Ibrahimovich kuhusishwa kujiunga na klabu ya Man Unitedzimechukua sura mpya, Zlatan anaripotiwa kukamilisha hatua ya nne ya kujiunga na klabu ya Manchester United.
    Dalili inayotajwa kuwa staa huyo yupo mbioni au katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Man United zinazidi kudhihirika, baada ya kuripotiwa tayari ametafutiwa nyumba ya kuishi katika jiji la Manchester ambapo ndio makao makuu au mji inapotoka klabu yaMan United.
    bgv
    Kwa mujibu wa nyaraka iliyopostiwa katika websites ya Proto Group Ltd ambao ni mawakala wa nyumba inaashiria kuwa mipango ya Zlatan kutangazwa kujiunga na Man United ipo tayari kutokana na mji alipotafutiwa nyumba ya kuishi, kwani kabla ya hapo alikuwa akiishi Paris Ufaransa.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Dalili nyingine ya Zlatan Ibrahimovic kuelekea kujiunga na Man United Rating: 5 Reviewed By: Anonymous
    Scroll to Top