Habari
hii imeripotiwa na BBC ambapo imesema Mahakama ya juu nchini Kenya
imehalalisha ngono baina ya mabinamu kwa sababu inakubalika katika
baadhi ya jamii nchini humo.
Hatua hiyo
imekuja baada ya Mahakama hiyo kumuachia huru mtu mmoja aliyekuwa
amefungwa kwa kosa la kushiriki ngono na binamu yake mwaka wa 2014 kwa
sababu sio makosa nchini Kenya. Jaji wa mahakama hiyo James Makau,
amesema katika maamuzi yake kuwa kujamiiana kwa maharimu sio haramu
nchini Kenya………
>>>’baadhi ya jamii nchini Kenya zinaruhusu sio tu ngono bali hata ndoa baina yao, jamii ya wahindi, waislamu na baadhi ya makabila humuhumu Kenya hukubali ndoa baina ya mabinamu’
Jamaa huyo alikamatwa mwaka 2014 kwa
kushiriki ngono na mpenzi wake wa kike ambaye pia ni binamu yake na
akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.Hukumu ya jaji Makau imedai kuwa ………>>>’Kwa ufupi hakuna ushahidi wowote uliotolewa kuthibitisha kuwa ngono baina ya wawili hao ni kinyume cha sheria na kwa sababu hiyo ninaamuru mtu huyo aachiwe huru mara moja’


0 comments:
Post a Comment