-Ni malumbano, visasi na kutoshirikiana tangu kuisha uchaguzi 2015
- Awataka wadumishe amani na kutii sheria
- Awahamasisha kujenga sekondari YA mfano ahahidi kuchangia na kushiriki ujenzi
- Rc, ukawa, Ccm wasakata sebene na kuanza maisha YA amani 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Amos Makalla leo ameweka historia katika kata YA Ndanto wilaya YA Rungwe
baada ya kumaliza msuguano wa kisiasa uliotokana na uchaguzi Mkuu mwaka
jana na kuifanya kata hiyo kuongozwa na Chadema lakini kwa muda mrefu
wanachama wenye mlengo tofauti na Diwani wamekuwa na msuguano mkali
kiasi cha shughuli za maendeleo kuzorota, Wafuasi wa vyama vya Siasa
kulumbana na kufikia kuchomeana ofisi, kungoa bendera na kutoshirikiana
ktk mambo YA kijamii

Kufuatia hali hiyo Mkuu
wa Mkoa amefanya mkutano wa hadhara na kukemea hali hiyo na kuwataka
wananchi hao kuacha malumbano na wajikite kwenye maendeleo zaidi na
ufundi wa Siasa waweke akiba mpaka mwaka 2020
Amewataka wananchi kumpa
ushirikiano Diwani kwakuwa amechaguliwa kisheria na akataka Diwani
kuwahudumia wananchi wote bila kuwabagua kwa itikadi zao
Amewataka kuvumiliana, kuheshimiana,
kupendana,kushirikiana
na serikali itawapa ushirikiano ktk shughuli zote za maendeleo na
amewataka kwa kuanzia waanze na ujenzi wa sekondari ya kata na Mkuu wa
Mkoa amehaidia kuwaunga Mkono kwa kuwachangia na kushiriki ujenzi jambo
lililoibua nderemo na vifijo na kufuatiwa na mziki maarufu disco la
nyimbo za Kisafa ambapo Rc, Diwani, Wafuasi wa Ccm , ukawa na wananchi
kucheza pamoja kuashiria kumalizika kwa Mgogoro 

Wananchi wengi wamepongeza jitihada za Mkuu wa Mkoa kwani tangu uchaguzi kata hiyo haijawahi kutembelewa na kiongozi

0 comments:
Post a Comment