Msanii
Snura ambaye mara nyingi amekuwa akikumbwa na rungu la BASATA kutokana
na video zake ambazo zinakuwa na utata, amesema mauno ambayo BASATA
'wanamind' ndio yamemfikisha hapo alipo.
Akiongea
kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Snura amesema mauno yake
ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuinua muziki wake, kutokana na
jinsi anavyoyamwaga akiwa jukwaani, na kuwavutia mashabiki wake.
"Nimeimba
sana laini kiuno changu kimenisaidia sana kunitambulisha, ukisikia kuna
show ya Snura jua mauno yanamwagwa kweli, na sijaanza leo nilianzia
kwenye ngoma za asili", alisema Snura.
Snura
aliendelea kusema kuwa ingawa mauno hayo humpa wakati mgumu akiwa
kwenye kazi zake kutokana na uchu wa baadhi ya wanaume wanaomsumbua,
lakini amekuwa akijitahidi sana kujilinda ili asiharibu kazi yake.
"Usumbufu
kiukweli upo,wengine wananipenda kweli wengine wananitamani, kikubwa
nazingatia sana kazi yangu, nashinda sana vishawishi kwa sababu vile
ninavyokatika wengine wanadhani nafanya promotion ya biashara", alisema
Snura


0 comments:
Post a Comment