Ripoti kuwa kampuni ya Apple imekuwa
ikitafakari kununua kampuni ya magari ya Uingereza McLaren kwa thamani
ya $1.5bn mpaka hivi sasa zimepuuziliwa mbali na pande zote mbili.
Lakini kuna sababu kadhaa zinazofanya taarifa hizo zitiliwe uzito.Kwanza, tumefahamu kwa muda sasa kuwa Apple inashughulikia teknolojia inayohusiana na magari.
Iwapo ni katika kupanga kuunda gari bado haijajulikana, lakini tunafahamu kwamba kampuni hiyo imekuwa ikiajiri na kuwafuta watu walio na utaalamu kuhusu magari kwa miaka kadhaa iliopita.
Tunajua kampuni hiyo inawekeza katika taaluma kutoka nje ikiwemo hudumu ya watu kukodi magari China Didi Chuxing yenye thamani ya $1bn iliyokithiri katika masoko hata huduma ya Uber ikaamua haina nafasi ya ushindani katika nchi hiyo.
"katika sekta ya viwanda vya magari kwa jumla, karibu kampuni zote zinatengeneza magari mapya katika kipindi cha kati ya miaka 7- 10 ," anasema Jim Holder kutoka jarida la Autocar.
McLaren ina wepesi zaidi ya kipindi hicho, anasema - jambo analoona litaivutia kampuni ya Apple.
Taarifa ya McLaren kuwa "haijadiliani na Apple kuhusu uwezekano wa uwekezaji wowote" iliambatana a kauli kuwa "kama unavyotarajia, kwa kiwango cha bidhaa zetu ina maana kuwa tunakuwa na mashauriano na washirika wengi, lakini hiyo ni siri".
Leo baadhi wanaona kama hilo linaashiria angalau kuanza kwa majadiliano yasio rasmi.
Mtazamo wa Apple wa kuficha siri unaamanisha tutajua wakati kampuni hiyo itakapokuwa tayari kutoa taarifa. Mradi huo bado ni mchanga - Tesla, Google na kampuni nyinginezo zina magari ambayo tayari yanahudumu.
Lakini pia, Apple haijawahi kuwa na wasiwasi wa kutokuwa wa kwanza, na washindani katika soko wanapaswa kutahadhari kwa yaliozipata kampuni kama Nokia na Blackberry.
0 comments:
Post a Comment