Vitunguu
ni zao la pili ambalo hutumika karibu kila siku katika mlo wa familia za
kitanzania. Afrika Mashariki, na Dunia Nzima.
Vitunguu
vina chukua nafasi kubwa katika matumizi ya mboga hasa kwa wakazi wa mijini.
Vitunguu hutumika katika kutengeneza kachumbari, kiungo cha mboga, nyama na
samaki. Majani ya kitunguu hutumika kama mboga. Vitunguu pia hutumika
kutengeneza supu n.k
Aina Za kilimo Cha Vitunguu
Aina Za kilimo Cha Vitunguu
Kilimo
cha vitunguu kinaweza kufanyika kwa aina mbili
- Green House
- Shambani
Kilimo cha kitunguu Green House
Kilimo cha vitunguu katika shamba la kawaida.
Zao la vitunguu hustawi vizuri kwenye maeneo
yasiyo na mvua nyingi sana, yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na yasiyo
na joto kali pamoja na ufukuto wa ukungu wakati wa kukomaa vitunguu.
Kutayarisha shamba
|
Shamba
litayarishwe sehemu usiyokuwa na mwinuko, sehemu ya wazi ambayo haijalimwa
vitunguu
kwa muda wa miaka 2 -3. Shamba liwe karibu na chanzo cha maji kwa ajili ya
umwagiliaji.
Matuta 1m x 3m au majaruba ya 2mx 3m.yanafaa kwa kupanda miche. Matatu au
majaruba
yanarahisisha umwagiliaji, palizi na unyunyiziaji wa dawa.
Upandaji
wa mbegu za vitunguu
Mbegu
zinaweza kupandwa kwa mstari au kwa kutawanya katika tuta la kitalu. Katika
upandaji wa mstari, mbegu hupandwa katika nafasi ya cm 10 hadi 15 kati ya
mstari na mstari. Baada ya kupanda, mbegu hufunikwa kwa udongo na baadaye kwa
kuweka matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu kuota, matandazo yaondolewe
na badala yake kichanja cha nyasi kijengwe ili kuiwekea kivuli mimea michanga.
Mbegu huota baada ya siku 7 hadi 10.
Matunzo
ya bustani ya vitunguu
- Umwagiliaji
Zao
la vitunguu linahitaji maji ya kutosha katika kipindi chote cha ukuaji wa mmea
na hasa wakati wa kutunga tunguu. Katika kipindi kisicho na mvua (mwezi mei
hadi Agosti) Umwagiliaji ufanyike mara moja kwa wiki kwa udongo wa mfinyanzi
tifutifu na vitunguu vilivyopandwa katika vijaruba. Ili kuharakisha kukomaa kwa
vitunguu unashauriwa kupunguza kiasi cha maji ya kumwagilia taratibu kadri zao
linavyo kua.
Pia
ni vizuri uache kumwagilia maji mapema wiki nne hadi sita kabla ya kuvuna.
Kwani muda kamili wa kukomaa na kuvuna kwa vitunguu ni siku 90 hadi 150
kutegemea na aina ya mbegu. Kuthibiti magugu na kupandishia udongo Kitunguu ni
zao lisilo weza kushindana na magugu. Magugu husababisha kupungua kwa ukubwa wa
kitunguu, hueneza magonjwa na husababisha kudumaa kwa vitunguu. Katika bustani
ya vitunguu, magugu yanaweza kutolewa kwa njia ya kutifulia kwa jembe dogo,
kung'olea kwa mkono na pia kwa kutumia madawa ya kuua magugu.
Kama
unaondoa magugu kwa kutifulia, epuka kutifua kwa kina kirefu ili kutoharibu
mizizi na vitunguu vyenyewe, kwani mizizi ya vitunguu ipo juu juu sana.
Kupandishia udongo kwenye mashina ya vitunguu ni hatua muhimu ili vitunguu
visiunguzwe na jua. Hakikisha kuwa mashina ya vitunguu vyako ndani ya
udongo kama sentimita 5. Pia kuna aina ya vitunguu ambavyo hutoa au
hupandisha tunguu lake juu ya udongo wakati vinapokua. Hivyo kupandishia udongo
ili kufunika tunguu ni muhimu sana.
Hali
ya hewa na maji
Hali
ya hewa na maji ni vipengele muhimu sana vya kuzingatia katika uzalishaji wa
vitunguu.
Vitunguu
vinastawi vizuri katika hali ya ukavu kwa kutumia umwagiliaji. Maji mengi hasa
wakati
wa masika inasababisha magonjwa mengi hasa ukungu, vitunguu haviwezi kukomaa
vizuri,
hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa mazao. Jua na hewa kavu ni muhimu sana
wakati
wa
kukomaa na kuvuna vitunguu.
Aina
za vitunguu
Aina
bora za vitunguu ni pamoja na Mang’ola red, Red creole na Bombay Red. Hizi ni mbegu bora
ambazo zinatoa mazao mengi kuanzia 40-60kgs kwa hekta. ikiwa kilimo bora
kitazingatiwa. Mkulima anaweza kuchagua mbegu kwa kuzingatia:-
- Mahitaji ya soko (vitunguu vyekundu hupendwa zaidi)
- Msimu wa kupanda
- Uwezo wa kuzaa mazao mengi
- Uwezo wa vitunguu kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
Mbegu bora
Ubora wa mbegu ni muhimu
sana, kwani ndiyo chanzo cha mazao bora. Mbegu bora inatoa miche yenye
afya na kuzaa mazao mengi na bora. Mbegu za vitunguu inapoteza uoto wake
upesi baada ya kuvunwa (mwaka1). Mbegu nzuri zina sifa zifuatazo:-
|
Hivyo
mkulima anaponunua mbegu za vitunguu azingatie yafuatayo:
- Chanzo cha mbegu
- Tarehe ya uzalishaji
- Tarehe ya kuisha muda wa
- Kifungashio cha mbegu.
Inashauriwa
mkulima asipande mbegu zenye umri zaidi ya mwaka mmoja
|
0 comments:
Post a Comment