Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amedokeza kuwa huenda akawania urais nchini mwake, Korea Kusini.
Muhula wake Ban kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa unakamilika mwisho wa mwezi huu wa Disemba Wakati wa mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari, Ban alisema kuwa baada ya kupata mapumziko anarudi nchini mwake Korea Kusini kuona vile ataisaidia nchi yake.
Uchaguzi wa uraia nchini Korea Kusini unatarajiwa kufanyika Desemba mwaka 2017
Lakini huenda uchaguzi huo ukafanyika katika muda wa miezi miwili baada ya bunge la nchi hiyo kupiga kura ya kumuondoa madarakani Rais Park Geun-hye, kutokana na sakata, ambapo analaumiwa kwa kumruhusu rafiki wake wa karibu kunufaika kifedha.
Ikiwa mahakama ya katiba itadumisha kura hiyo ya kumuondoa, atakuwa rais wa kwanza wa Korea Kusini aliye madarakani kuondelwa katika kipindi cha uhuru wa nchi hiyo.
Mahakama ya katiba ina siku 180 kutoa uamuzi wa mwisho.
Matamshi ya Ban yanakuja huku yakishuhudiwa maandamano kwenye mji mkuu wa Korea Kusini, Seol.
Chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment