Rais wa Marekani Barack Obama
amesema kuwa alimuamrisha rais wa Urusi Vladimir Putin kusitisha udukuzi
wa mitandao kabla ya kufanyika uchaguzi nchini Marekani.
Akimaanisha kuwa rais wa Urusi alielewa udukuzi huo, bwana Obama alisema kuwa, si mengi yanafannyika Urusi bila Putin Kuhusika. Obama alisema kuwa alikuwa amemuounya Putin kuhusu hatua kali wakati wa mkutano wa mwezi Septemba.
Mwezi mmoja baaadaye Marekani iliilaumu Urusi kwa kuingilia masuala yake ya kisiasa.
Obama ameahidi kujibu vikalia udukuzi huo uliolenga chama cha Democratic na parua pepe za mwenyekiti wa kampuni ya mgombea urais Hillary Clinton.
Rais Obama hakumlaumu mrithi wake, Donald Trump wala kumtaja jina, lakini amesrma kuwa baadhi ya warepublican wameshindwa kuona atharia za kuhusika kwa Urusi katika uchaguzi wa Marekani.
Mapema wiki hii Donald Trump alikashifu madai ya mashirika ya ujasusi ya Marekani kuwa wadukuzi wa Urusi walisaidia kushawishi matokeo ya uchaguzi wa Marekani.
Hata hivyo Urusi imekana madai hayo.
Chanzo:BBC
0 comments:
Post a Comment