Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu
nchini Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi alipowasili katika ofisi za
ubalozi huo kushiriki sherehe ya madhimisho ya miaka 45 ya
muungano.Tanzania na UAE zimepiga hatua kubwa za ushirikiano hususan ya
kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) hadi
Juni, 2015 makampuni 67 ya uwekezaji kutoka UAE yamewekeza hapa nchini
katika sekta mbalimbali wenye thamani ya USD 497.12 Millioni na kuajiri
Watanzania 9,044. Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu unaundwa na falme
saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah,
Ajman na Umm al-Quwain .
Rais
Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi
wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 45 ya muungano wa falme hizo .
Mhe.Waziri Balozi Dkt.Mahiga akivalishwa skafu maalum
Mhe.Waziri Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi
Wageni waalikwa wakifuatilia jambo
Balozi wa Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi akizungumza wakati wa maadhimisho
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga akitoa hutuba fupi wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdalla Kilima akisalimiana na Mhe. Balozi wakati wa sherehe za maadhimisho
-----------------------------------------------------------
Tanzania
na Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) zimepiga hatua kubwa za ushirikiano
hususan wa kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) hadi Juni, 2015 Makampuni 67 kutoka UAE yamewekeza hapa nchini
katika sekta mbalimbali kwa mtaji wa thamani ya Dola za Marekani milioni
497.12 na kuajiri Watanzania zaidi ya 9,044.
Hayo
yalibainishwa jana katika sherehe za kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya UAE
zilizofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alikuwa
Mgeni Rasmi.
Tanzania
na UAE zinatarajiwa kufanya Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya
Kudumu ya Ushirikiano (JPC) ambao utakuwa chachu ya kuimarisha mahusiano
baina ya nchi hizi mbili hususan ya kiuchumi.
Akiongea
katika hafla hiyo, Mhe. Waziri alilipongeza taifa hilo kwa kuadhimisha
siku yake ya Kitaifa ikiwa imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo ya
kichumi, kijamii na kisiasa. Mhe. Waziri alisema kuwa siku hiyo ni
inatoa fursa pia ya kutathmini mahusiano mazuri yaliyopo baina ya
Tanzania na UAE.
Kwa
upande wake, Balozi wa UAE hapa nchini, Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim
Alsuwaidi aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa
inayotoa kwa Ubalozi huo ambao unamwezesha kutekeleza majukumu yake kwa
wepesi ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili. Mhe.
Balozi aliahidi kuendeleza ushirikiano huo hususan katika kutimiza azma
ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unajumusha falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain huadhimisha siku yake ya Kitaifa tarehe 02 Disemba ya kila mwaka tokea mwaka 1971.
0 comments:
Post a Comment