Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (katikati) akisaini Mkataba kwa niaba ya Serikali na Klabu ya
Yanga ya jijini Dar es salaam ambayo iliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu
wa Klabu hiyo Baraka Deusdedit (kulia) leo jijini Dar es salaam. Mkataba
huo unahusu Klabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na Uwanja wa
Uhuru katika mechi za Kimataifa na Ligi Kuu. Wa kwanza kushoto ni Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Evordy Kyando.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akibadilishana Mkataba waliosaini na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu
ya Yanga Baraka Deusdedit leo jijini Dar es salaam. Mkataba
huo unahusu Kalabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na Uwanja wa
Uhuru, Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge.
Picha
ya pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) mara baada ya kusaini
Mkataba na Klabu ya Yanga leo jijini Dar es salaam. Wa pili kulia ni
Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit.
Na Eleuteri Mangi – WHUSM.
Serikali
imesaini Mkataba na Klabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa pamoja
na Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya michezo yote ya Kimataifa pamoja na
michezo ya Ligi Kuu ya ndani.
Mkataba
huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kwa niaba
ya Serikali na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit kwa
niaba ya Klabu ya Yanga.
Katika
Mkataba huo, Klabu ya Yanga imeruhusiwa kutumia viwanja hivyo kama
viwanja vyake vya nyumbani kwa sharti la kuvitunza viwanja hivyo wakati
wote wanapovitumia.
Miongoni
mwa masharti hayo ni kutunza viwanja, mali na vifaa vyote vilivyopo
katika viwanja hivyo, na endapo kutatokea uharibifu wowote utakaofanywa
na wachezaji ama mashabiki, Klabu hiyo itawajibika kubeba gharama za
matengenezo yote yatakayotokana na uharibifu huo.
Aidha, Klabu ya Yanga inaweza kutumia viwanja hivyo kwa mazoezi ya kujianadaa na mechi zinazowakabili.
0 comments:
Post a Comment