Mara
nyingi mwili ukichoka watu wengi wanapenda kufanya massage ili kuondoa
uchovu, unaambiwa kuwa wageni wanaotembelea mji wa Cebu Zoo huko
Philippines, wanafurahia huduma mpya ya kufanya massage ambayo
inatolewa na nyoka wanne aina ya chatu ambao huuzunguka mwili wote.
Ufanyaji
massage kwa kutumia nyoka ni Biashara ambayo iko serious huku nyoka
wanaotakiwa kutoa huduma hiyo lazima wawe na urefu wa mita tano na
uzito wa 250kg, biashara ambayo awali ilikuwa ikifanyika bure katika mji
wa Cebu Zoo kabla haijawa maarufu na kutumiwa na watu wengi.
Msimamizi
wa mji huo Giovanni Romarate amesema wakati wanaanza biashara hiyo
wageni walikuwa wanaogopa, lakini wengi waliojaribu waliipenda na sasa
hutolewa kwa kulipia na mchango unaopatikana husaidia maendeleo katika
mji huo.
Unaweza kutazama Video hiyo hapa kwa kubonyeza play mtu wangu.