MABINGWA mara nne wa kombe la
Mataifa ya Afrika, timu ya taifa ya Ghana imepoteza mechi yake ya kwanza
ya kundi C ya michuano ya Mataifa ya Afrika inayoendelea Guinea ya
Ikweta kwa kufungwa bao 2-1 na Senegal.
Dakika za mapema (dk 14’) Andre
Ayew aliifungia bao la kuongoza Ghana kabla ya Simba Wateranga
kusawazisha katika dakika ya Mame Biram Diouf katika dakika ya 58’.
Moussa Sow aliwanyanyua mashabiki wa Senegal katika dakika ya 90’ akiandika bao la kuongoza.
Mechi ya pili ya kundi C imemalizika usiku huu kwa Algeria kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Afrika kusini.
Huu ni ushindi wa kwanza mkubwa katika mechi sita zilizocheza.
Afrika kusini walikuwa wa kwanza
kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 51’ kupitia kwa Thuso Phala,
lakini Algeria walifuta bao hilo dakika ya 68’ kutokana na Thulani
Hlatshwayo kujifunga.
Dakika ya 72’ Faouzi Ghoulam aliiandika bao la pili Algeria na baadaye Islam Slimani alihitimisha sherehe ya ushindi.
Gabon walipata matokeo ya bao 2-0
dhidi ya Burkina Faso. Timu ya pili kupata ushindi mwingine imekuwa
Senegal ambayo imeshinda 2-1.
Guinea ya Ikweta wao walitoka sare ya 1-1 katika mechi ya kundi A, wakati kundi B timu zote zilitoka sare.
Zambia walitoka sare ya 1-1 na DR Congo baadaye Tunisi walitoka 1-1 na Cape Verde.
MATOKEO YA MECHI ZA KUNDI C
| Africa Cup of Nations – Group CJanuary 19 | |||
|---|---|---|---|
| FT | Ghana | 1 – 2 | Senegal |
| FT | Algeria | 3 – 1 | South Africa |
Baada ya kundi kundi C kucheza
mechi za ufunguzi, leo ni zamu ya kundi D ambapo Tembo wa Pwani ya
Magharibi mwa Afrika, Ivory Coast watashuka dimbani kuchuana na Guinea
majira ya saa 1:00 usiku.
Mechi ya pili itapigwa majira ya saa 4:00 usiku ambapo Mali wataivaa Cameroon.
RATIBA YA LEO AFCON KUNDI D
| Africa Cup of Nations – Group DJanuary 20 | |||
|---|---|---|---|
| 19:00 | Ivory Coast | ? – ? | Guinea |
| 22:00 | Mali | ? – ? | Cameroon |

