Ivory Coast imeitwanga Algeria kwa mabao 3-1
katika mechi ya Kombe la Mataifa Afrika hatua ya robo fainali.
Mabao mawili ya Bony Wilfred aliyejiunga na Manchester
City akitokea Swansea na moja la Gervinho yalitosha kuizima Algeria
iliyoonyesha soka safi.
Hata hivyo haikuwa kazi lahisi, kwani pamoja na
Tembo hao kuanza kufunga, lakini Algeria walisawazisha na kuwapa wakati mgumu
Waafrika hao wa Magharibi.
Uwezo wa wachezaji mmojammoja kwa Ivory Coast pia ulichangia kuongeza uwezo wa kikosi hicho ambacho sasa kitakutana na DR Congo katika mechi ya nusu fainali.