Ofisa
Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akifafanua jambo wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa matibabu ya watoto 400 wenye
matatizo ya kupinda miguu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi
Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya kusaidia matibabu ya watoto 400 wenye matatizo ya kupinda
miguu. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya kupinda miguu katika
mpango wake wa kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na
ugonjwa huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania,
Ammish Owusu-Amoah.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akionyesha picha za watoto wenye
matatizo ya kupinda miguu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa
dola 100,000 ili kuisaidia matibabu ya watoto 400 wenye matatizo
yakupida miguu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania,
Ammish Owusu-Amoah.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akionyesha picha za watoto wenye
matatizo ya kupinda miguu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa
dola 100,000 ili kuisaidia Hospitali ya CCBRT katika mpango wake wa
kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa huo.
NA FRANCIS DANDE
BANK
OF AFRICA-TANZANIA, leo imezindua rasmi kampeni ya uchangiaji wa dola
100,000 ili kuisaidia Hospitali ya CCBRT katika mpango wake wa
kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kupinda
miguu.
Msaada
huu kwa Hospitali ya CCBRT utawezesha watoto kutoka katika mikoa
mbalimbali ya Tanzania kupata matibabu bure au kwa gharama nafuu ili
kuwawezesha kutembea sawa sawa.
Ugonjwa wa kupinda miguu unaweza kuathiri mguu mmoja au yote miwili. Miguu iliyopinda huonekana kuingia ndani hasa katika goti.
Bila
kupatiwa matibabu, wagonjwa wa aina hii mara nyingi hutembea kwa
kutumia magoti au au pande wa pili wa nyayo zao, lakini wakipatiwa
matibabu mapema wakati wa utotoni watoto hao huweza kutembea vema na
hata kushiriki mchezo wa riadha.
Katika
taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa BANK OF AFRICA-TANZANIA, Owusu-
Amoah, alisema benki yake itaendelea kuisaidia CCBRT kwa kila hali,
ikiwamo hilo suala la matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa kupinda
miguu ili kuboresha maisha ya Watanzania.
Kwa
upande wake, Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemann, alisema kuwa CCBRT
imekusudia kuyabadili maisha ya Watanzania, lakini hawatafanikiwa
kufikia lengo lao bila kupata msaada kutoka kwa washirika wakarimu kama
BANK OF AFRICA-TANZANIA.
“Kwa
kusaidia matibabu ya ya ugonjwa wa kupinda miguu, BANK OF
AFRICA-TANZANIA itasaidia kuzuia ulemavu miongoni mwa mamia ya watoto,
hivyo kuboresha nmaisha yao,” alisema Telemann.
Kampeni
hiyo itahusisha wafanyakazi wa benki hiyo hapa nchini, wateja na wale
wote wanaosambaza bidhaa mbalimbali kwao.Telemann aliongeza kuwa dhamira
hii itasaidia kuhakikisha watoto wetu wanakuwa na maisha bora siku za
baadaye na kuzifikia ndoto zao.
Vilevile kutasaidia kujenga jamii iliyo imarika kiafya, yakiwamo maisha ya wenye ulemavu.

