Eneo la machimbo
ya madogo ya dhahabu ya kijiji cha Kalole kata ya Runguya tarafa ya
Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Mpaka sasa inadaiwa
wachimbaji wadogo wadogo 19 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya
kufunikwa na kifusi kufuatia wa mvua zinazoendelea kunyesha na
kusababisha kubomoka kwa mashimo hayo katika machimbo madogo ya dhahabu
ya kijiji cha Kalole kata ya Runguya tarafa ya Msalala wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa kamanda wa
polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema waliofariki dunia ni
watu 19 ambapo usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivamia
machimbo hayo ambayo yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza
shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa
imara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakabomoka na
kuwafukia na kusababisha vifo vyao.
Baadhi ya duara ya simo la kuchimba dhahabu katika kijiji cha Kalole wilayani Kahama mkoani Shinyanga.