Tukio
hilo lilitokea Aprili 18, mwaka huu, maeneo ya Mkuranga mkoani Pwani
ambapo awali familia hiyo ilipata taarifa kuwa kuna watu wanaonekana
kwenye shamba lao wakikata miti na kujipimia maeneo, hali iliyowalazimu
kufunga safari ili kujua watu hao walikuwa na lengo gani.
Akizungumza
na waandishi wetu, Karim alisema kuwa akiwa shambani hapo na mkewe
pamoja na marafiki wengine wawili, watu hao waliotajwa kama wavamizi
waliwafuata na kuwauliza walifuata nini shambani kwao huku wakiitana kwa
miluzi, kitendo kilichowafanya waongezeke na kuwazunguka huku wakiwa na
mapanga, fimbo na visu ambavyo vilitumika kuwapiga navyo.
“Walikuwa
si chini ya 30, walitupiga sana na mabapa ya mapanga wengine kutukata
nayo baadaye wakapekua mifukoni na kutulazimisha kuwapa vitambulisho
vyetu. Walitupokonya na fedha kiasi cha shilingi 780,000/= ambazo
zilikuwa nyumbani kwangu,” alidai Karim.
Naye mke
wa Karim aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Omary, alisema kuwa yeye na
mfanyakazi wake walivamiwa wakiwa ndani ya nyumba yao iliyopo hukohuko
shambani ambapo wavamizi hao walikuwa wakiongea Kikurya na kuwataka
wafungue mlango ambao waliufungua baada ya kutishiwa kuuvunja.
“Baada ya
kufungua walianza kutupiga kwa mabapa ya mapanga na mwenzangu walimkata
mkono, wenyewe walidai shamba hilo ni la ndugu yao na siyo letu,
nilipowabishia kwa ushahidi walizidi kutupiga na wakapekua na
kutupokonya simu zetu na fedha tulizokuwa nazo, kama hiyo haitoshi
walianza kutudhalilisha.
“Baadaye
nilimuona mume wangu na wenzangu wakiletwa wakiwa wameloa damu. Wakasema
watatuchoma moto na wakachukua petroli na kuanza kumwaga ndani, lakini
rafiki yangu niliyeenda naye alikuwa ni Mkurya; akaanza kuwaomba kwa
lugha ya kwao lakini hawakumuelewa,” alisema Aisha.
Aliongeza
kuwa baadaye mmoja wao aliwaambia wenzake wawatoe nyumbani hapo na
kuwataka wasirudi tena katika eneo hilo ndipo walikwenda Kituo cha
Polisi cha Vikindu na kupewa hati ya kuwawezesha kutibiwa (PF3) na
likafunguliwa jalada la kesi lililosomeka VK/RB/280/15 KUTISHIA KUUAWA
KWA SILAHA na baadaye Kituo cha Polisi cha Mbagala, Kizuiani Dar ambapo
walifungua jalada la kesi MBL/RB/3805/2015 KUJERUHI.
Akizungumza na waandishi wetu, Afisa mtendaji wa Kata ya Tambani, Abasi Shabani alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza:
“Tayari
jeshi la polisi limeshachukua hatua kwa kwenda eneo la tukio na hali ya
eneo kwa sasa imekuwa shwari kwa kuwa kuna baadhi ya watu tayari
wanashikiliwa wakihusishwa na tukio hilo