Habari
zilizotufikia muda huu wa saa nane mchana ni kuwa hadi sasa imeelezwa
kuwa watu sita (6) wamepoteza maisha kufuatia ajali ya basi la abiria la
Nganga lililogongana na Fuso, na kupelekea magai hayo kuwaka moto,
katika eneo la Ruaha Mbuyuni mpakani kwa Morogoro na Iringa.
Hata
hivyo, bado kuna ugumu wa habari kamili kutokana na umbali wa eneo hilo
la tukio huku tukihalifiwa kuwa, makamanda wa jeshi la Polisi wa
Morogoro na Iringa wote simu zao hazipatikani kwa muda mrefu. Ambapo pia
kutokana na ufinyu wa bajeti kwa baadhi ya vyombo vya habari,
wameshindwa kufika kwa wakati kwenye eneo la tukio kutokana na kuwa
mbali na miji mikuu ya mikoa hiyo ya Iringa na Mbeya.
Kwa
mujibu wa ripota wetu kutoka Mkoa wa Morogoro alibainisha kuwa, karibu
wandishi wengi wameshindwa kuelekea eneo la tukio kutokana na vyombo
vyao kutokuwa na mafuta ya kutosha huku hapo hapo Ofisi za jeshi hilo la
Polisi kwa siku ya leo nyingi zikiwa zimefungwa.
MODEWJI: Hallo!!: Hapo Morogoro tupeni Habari. vipi kuhusiana na ajali ya Ruaha Mbuyuni!.
RIPOTA
MOROGORO: “Ni kweli lakini sote tunataka kwennda lakini tumeshindwa
huko ni mbali sana.. kutoka hapa Morogoro Mjini hadi hapo ni zaidi ya
KM110 ambazo tu unaimaliza mbuga ya Mikumi, ukitoka hapo uanze
kuitaafuta Mbuyuni ni zaidi ya KM 35, hivi?.
Unafikiri ni karibu? tumeshindwa hata magari ya abiria tunayoomba lifti, kwa muda huu tutachelewa tu”. Kilieleza chanzo hicho.
Chanzo
hicho pia kilibainisha kuwa, kutokana na ajari hiyo kutokea katikati ya
mpaka wa Morogoro na Iringa, majeruhi wanaweza kupelekwa Hospitali
iliyopo Mikumi ama Iringa mjini.
Modewji
ilipowasiliana na ripota wa kujitegemea Mkoani Iringa, alibainisha
kuwa, hadi sasa bado wanaendelea kukusanya taarifa ila walioweza
kupoteza maisha hapo hapo ni sita, akiwemo pamoja na dereva wa Fuso.
Picha
ambazo zimeweza kupatikana ni kwa msaada wa teknolojia ya simu za
kisasa zenye uwezo wa kupiga picha na kurusha kwa kutumia intaneti
(tehama/ICT) hivyo tunapongeza kwa teknolojia hii na kwa wale walioweza
kutuma picha hizi ambazo kwa asilimia kubwa hazikukiuka maadili.
..credit ziende kwa waliopiga hizi picha za ajali, Pia Modewji blog
inatoa pole kwa wale wote walioondokewa na wapendwa wao, waliojeruhiwa
na kupata matatizo kwenye ajali hiyo.
Modewji blog, tunaendelea kuwasiliana na vyanzo zaidi ilikukupatia abari iliyo bora, endelea kuperuzi nasi.
HABARI KWA HISANI YA MO BLOG