Moja ya
story kubwa kuripotiwa na kituo cha ITV jioni hii ni ishu ya watoto
watatu wa kiume kukutwa wakiwa wamejificha kwenye chasis ya basi.
Watoto hao wamekutwa Singida ambapo tayari walikuwa wamesafiri kutoka Kahama na walikuwa wakielekea Arusha.
Watoto
hao wamesema walitolewa na mtu mmoja Arusha kwenda Kahama akawaambia
kuna kazi, walipofika Kahama akawatelekeza, baadae wakaamua kurudi kwa
njia hiyo ya kujificha kwenye chasis ya basi.
Kamanda
wa Polisi Singida ACP Thobias Sedoyeka amesema watoto hao walikutwa
wakati wakaguzi wa mabasi walipokuwa wakikagua basi hilo laMgamba
Express ambapo mpaka wanafika hapo basi lilikuwa limesafiri kwa zaidi ya
Kilometa 360.

