Afisa Habari Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Rose Mdami (kulia) akitoa maelezo kwa
mmoja wa wageni waliotembelea banda la Mamlaka hiyo kuhusu huduma
zinazotolewa na Mamlaka hiyo, katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jjijini Dar es
Salaam.
Mwananchi aliyetembelea Banda la
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), akipewa maelezo na Afisa
Habari Mkuu wa Mamlaka hiyo, Rose Mdami (kulia) kuhusu taarifa
mbalimbali zinazoandaliwa na Mamlaka hiyo, katika maonyesho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja,jijini Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Polisi
nchini,Tumaini Julius, akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea
banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu shughuli mbalimbali
zinazofanywa na Jeshi hilo, katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa
Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jjijini Dar es
Salaam.
Mmoja wa wananchi waliotembelea
banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akipiga picha na sanamu
la askari linaloonyesha mavazi yaliyokuwa yanavaliwa na askari wa
kike, katika maonesho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanaendelea
katika viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi Msaidizi wa Idara ya
Uhamiaji, Dickson Rweza (kushoto), akitoa maelezo kwa mmoja wa
wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
katika maonesho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanaendelea katika
viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.