Kanisa la Wamarekani wenye asili ya
Afrika ambalo waumini wake tisa waliuwawa huko South Carolina
litafunguliwa tena kwa ibada ya jumapili kuanzi leo.
Wafuasi wa kanisa hilo la Emanuel
AME walikutana jana katika chumba ambacho wenzao waliuwawa kwa
kupigwa risasi na kijana mweupe siku ya jumatano.
Wakati huo huo polisi wanachunguza
posti iliyotumwa mtandaoni, inayoshukiwa kuwa ni ya kijana huyo
ambayo inaelezea kilichomsukuma kufanya kitendo hicho.