Maafisa usalama nchini Burundi
wamesema polisi 11 wamejeruhiwa katika matukio ya kushambuliwa kwa
mabomu ya kutupwa kwa mkono yaliyotokea Jijini Bunjumbura.
Milipuko na milio ya risasi
imesikika katika maeneo mbalimbali ya Jiji hilo wakati wa mashambulio
hayo yaliyofanywa kwa kufuatana kwenye vituo vya polisi vya na kwenye
gari.
Mashambulio hayo yametokea katika
wilaya ambazo zimeshuhudia maandamano dhidi ya rais Pierre
Nkurunziza kutokana na uamuzi wake wa kuwania urais kwa muhula wa
tatu.