Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
amewaongoza maelfu ya watu katika programu ya mazoezi ya yoga kwenye
Jiji Kuu la Delhi nchini India wakati wa maadhimisho ya kwanza ya
siku ya Kimataifa ya Yoga kufanyika nchini humo.
Bw. Modi alifanya mazoezi ya
kunyoosha viungo, kuinama pamoja na ya kupumua akiwa pamoja na
wanafunzi 35,000 maafisa wa serikali na wanajeshi wa India.
Usalama uliimarishwa katika jiji
hilo kwa maelfu ya polisi na vikosi vya jeshi kuwekwa katika tukio
hilo lililofanyika leo asubuhi.
Mamilioni ya watu wanatarajiwa
kufanya mazoezi ya yoga katika hafla kama hiyo kwenye mamia ya majiji
na miji ya nchini India.