Kukiwa kumesalia mizi miwili na siku kadhaa kabla ya ligi kuu ya England na lingi nyingine kubwa barani ulaya kuanza mpira rasmi utakaotumika kwenye ligi ya England umefahamika .
Mpira huo umebuniwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Kimarekani ya Nike ambapo utakuwa unafahamika kwa jina la Nike Ordem na umetengenezwa kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa ambayo inaendana na mabadiliko ya mchezo wa soka .
Mpira huo umetengenezwa kwa kuzingatia jinsi ambavyo wachezaji watakuwa wakiutumia uwanjani ambapo moja ya vitu vilivyozingatiwa ni rangi yake na umetengenezwa kwa rangi angavu ili kuwasaidia wachezaji kuuona wakiwa uwanjani na kufanya maamuzi ya haraka.
Mpira huo pia una sehemu 12 ambazo zinaufunika ili kuusaidia kwenda na kasi ambayo itawasaidia wachezaji wenye uwezo wa kupiga mashuti ya mbali .
Mpira huo ambao unatarajiwa kuzinduliwa mwezi julai pia utatumika kwenye ligi za Hispania na Italia na umeonekana ukifanyiwa majaribio na wachezaji wa klabu ya West Ham United kwenye uwanja wao wa mazoezi .